Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Tuesday, 13 June 2017
Friday, 17 July 2015
Thursday, 16 July 2015
Sunday, 26 April 2015
MAFUNZO ELEKEZI BVR IRINGA.
Neni Guvette akitoa maelekezo kwa maafisa waandishaji matumuzi ya BVR ilinao wakawafundishe waandishaji wasaidizi katika katazao wilayani wanakotoka. Mnyalu.
Maafisa waandikishaji wilaya ya Iringa wakifanyazoezi la upigaji picha kwakutumia Mashine ya BVR wakati wa mafunzo yalioishajana Mkoa wa Iringa. Mnyalu.
Maafisa waandikishaji wilaya ya Iringa wakifanyazoezi la upigaji picha kwakutumia Mashine ya BVR wakati wa mafunzo yalioishajana Mkoa wa Iringa. Mnyalu.
MAEUNZO KWA MAAFISA WAANDISHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGAKURA IRINGA SASA.
Afisa muwezeshaji toka Nec taifa Sanif Khalfani akitoa maelekezo ya namna ya Kutumia Mashine ya Kielektronik BVR kwa Maafisa waandikishaji Daftari la wapigakura la kudumu Mkoa wa Iringa. kwa maandalizi ya kuanza rasmi uandikishaji mkoamzima kwa kuanza na baadhi ya vutuo kwa uhaba wa Vifaa vya BVR. Mnyalu.
Thursday, 9 April 2015
UCHAMBUZI WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015
UCHAMBUZI WA SHERIA YA MAKOSA YA
MTANDAO, 2015
UTANGULIZI
UTANGULIZI
Sheria hii ya Makosa ya Jinai kupitia Mtandao, 2015 ina mapungufu mengi. Mapungufu hayo yamebainika kuwa, kama sheria ikipita yanaweza kuifanya nchi ikawa ni kati nchi adui za matumizi ya mtandao wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano duniani.
Watanzania wote wanatakiwa kufahamu kuwa muswada ukipita utatumika nchini kote yani Tanzania Bara na Visiwani.
Watanzania walio wengi hawafahamu Sheria hii inawahusu kwa namna gani; lakini kwa lugha rahisi ni kuwa itamuathiri mtu yeyote anayeweza tumia Mtandao wa Intaneti kwa kutimia kifaa chochote iwe kompyuta kubwa au vifaa vyenye uwezo wa kufanya kazi kama kompyuta kama Simu za mikononi, saa, televisheni na vifaa vingine vinavyoendana na hivyo.
Malengo ya Sheria hii ni kuainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kielektroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.
Matumizi ya mitandao yote mikubwa kama Twitter, Instagram, JamiiForums, Facebook, Barua pepe, WhatsApp, blogu na data zote zilizo katika kifaa chochote cha kielektroniki yanaathiriwa kwa kiwango kikubwa na Muswada huu.
UCHAMBUZI
Kifungu cha 7
(1-3): Haibainisha ni aina gani za data ambazo haziruhusiwi kuguswa/kufutwa au zikiguswa/futwa ni kosa la jinai.
7(1g): Kipengele hiki katika kifungu hiki kinarudiwa mara kadhaa katika (Vifungu vya 32-35). Badala ya vifungu vya mbele kurejea kifungu hiki, watunga sheria wameiacha kifungu hiki kikiwa hakieleweki hadi mtu asome vifungu vya mbele.
Je mtu aliyeidhinishwa katika ibara na kipengele hiki ni nani?
Kifungu cha 8:
Muswada huu haujaweka bayana iwapo nyaraka za siri zinaweza kuwekwa wazi katika mtandao kama zina maslahi ya nchi au wananchi mf. Matumizi mabovu ya pesa za umma
Kifungu cha 14:
Neno pornografia halijapewa maana na hivyo jambo lolote lenye mwonekano wa kiasherati (sexually vulgar) linaweza kutafsiriwa kama pornografia na kumuingiza muhusika matatizoni.
Ponografia ya mtandao isikatazwe kabisa ila inatakiwa kuweka ulinzi thabiti wa kuhakikisha watoto hawawezi kufungua mitandao ya aina hiyo.
Ponografia zote ni chafu lakini sio chafu zote ni ponorafia. Hivyo kutokana na kuwa sheria hii inasema ponografia zote ni chafu hii itasababisha kila mtu ahukumiwe chini ya kifungu B.
Uchafu na Ponografia viwe vipengele viwili tofauti.
Kifungu cha 15:
Suala la kujifanya mtu mwingine kwenye mtandao, linaweza kuleta utata kwani kuna baadhi ya mitandao ambapo watumiaji hutumia majina ambayo sio ya kwao. Itakuwaje watu kwa madhumuni mabaya wakitafuta mtu mwenye jina kama hilo na kumshtaki mtumiaji wa mtandao?
Je, mtu kujifanya mtu mwingine inahusisha mtu kutumia jina lisilo lake hata kama hajajifanya mtu mwingine? Ni vema suala hili likafafanuliwa kisheria kwakuwa ni suala muhimu lakini wachache wataelewa manaa yake.
Kifungu cha 16:
Ni nani ana mamlaka ya kubainisha kuwa jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la UKWELI, UONGO au UPOTOSHAJI? Ni wazi kuwa mamlaka husika inaweza tumia hili kama mtego kwa manufaa yao.
Kipengele hiki kama vingine kimeambatanisha muda usiopungua bila kusema muda usiozidi. Hivyo mtuhumiwa anaweza kufungwa hata kifungo cha maisha kutokana na mamlaka ya mahakama.
Watu binafsi wanaweza kutumia vibaya kifungu hiki kuzuia uhuru wa maoni kwa kuwaburuza watumiaji wa mtandao mahakamani kila kukicha na kuwapotezea muda wahusika ambao wanaweza kubainika mwishoni kuwa walionewa.
Kifungu cha 20:
Katika mawasililano ya mtandao kama ilivyo mawasiliano mengine kuna ujumbe ambao mtu hawezi kuacha kuupata
Mfano kutembea barabarani na kuona bango la matangazo, au kuwa ndani ya daladala iliyowasha redio.
Vivyo hivyo katika mtandao sio kila ujumbe anaopokea mpokeaji ameuomba na hivyo kifungu hiki kinafanya kila mtu atakayepokea ujumbe bila ridhaa yake kuwa amefanya kosa la jinai.
Kifungu cha 21(1):
Tafsiri za Kiswahili na kiingereza zipo tofauti kabisa.
Tuesday, 2 December 2014
Saturday, 24 May 2014
Thursday, 15 May 2014
SHULE ZA SEKONDARI ZILIZO FANYA VIZURI KITAIFA MUFINDI ZA ZAWADIWA.
Mkuu wa Wilaya Mufindi Evarista kalalu akimkabidhi Sr Jeslin Sabs Cheti cha Ufauru pamoja na Ngao kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Bethel Sabs Mafinga kwa kushika nafasi ya 7 kitaifa kwa ufauru ikiwa na Idadi ya wanafunzi chini ya Arobaini hafra hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Halmashauri Mufindi chini ya Wizara ya Elimu na mafunzo ua ufundi.Tanzania. Mnyalu.
Wednesday, 14 May 2014
MB MUFINDI KASKAZINI ATOA VIFAA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Evarista kalalu akikabidhi Kompyuta mbili Paulo Mahimbi Mw /Mkuu shule ya Msingi Ugesa moja kati ya Kompyuta 5 zilizo tolewa na Mh Mahammod Mgimwa. Mnyalu.
Iringa.Halimashauri ya wilaya ya mufindi inakabiliwa na
upungufu wa madawati 4269 kwa uwiano wa dawati moja kwa wanafunzi wawili wakati
awali wilaya hiyo ilikuwa ikisifika kwa utumiaji wa madawati ya Adobe licha
ya wilaya hiyo kuvuna mbao.
Hayo yalibainishwa juzi wakati wakipokea madawati 100 na kompyuta 5 zenye thamani ya shilingi
mil 12 kutoka kwa Naibu waziri wa maliasili na utalii Mh Mohamud Mgimwa ambaye
pia ni mbunge wa jimbo la mufindi kasikazini kwa kushirikiana na mfuko wa
penseni kwa watumishi wa uma(PSPF) Iringa.
Mgeni rasimi
katika makabidhiano hayo mkuu wa wilaya ya mufindi Evarista Kalalu alisema kuwa
wilaya ya Mufindi haina upungufu wa madawati kwa uwiano wa dawati moja kwa
wanafunzi wawili upungufu uliopo niwa walimu wa sayansi kitendo kinacho
sababisha kutokuanya vizuri katika somo hilo.
“Wakuu wa shule kwa kuwa mufindi haina upungufu wa
madawati upungufu uliopo ni wa walimu wa sayansi hivyo nawaombeni masomo
yaliyosalia yaweze kuleta matokeo mazuri shuleni”alisema Kalalu
Kwa upande wake Afisa elimu msingi Mufindi Farida
Mwasumilwe alisema kuwa wanashukuru kupokea vifaa hivyo kwa sababu wanahitaji
kuboresha ili uwiano uwe kwa dawati moja kwa mwanafunzi mmoja ili waweze
kujitegemea katika mtihani wa mwisho.
“Nawashukuru wadau mbali mbali ambao wanajitokeza
katika kuweka nguvu katika sekta ya elimu na madawati haya yanaenda katika
shule ya msingi mjimwema,Mamba,
nyamalala na kompyuta zinaenda
shule za msingi Ugesa, Itona na
Igombavanu sekondali.”alisema Farida
Naye Baraka Jumanne Ofisa mfawidhi mkuu wa PSPF Iringa aliwataka walimu hao pamoja na
wanafunzi kuvitunza vifaa hivyo ili vidumu na vitumike kwa wanafunzi wengine
wanaotarajiwa kuanza masomo.
Mnyalu.
MWISHO.
Tuesday, 13 May 2014
MBUNGE MUFINDI KASKAZINI ATOA VIFAA SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI MUFINDI KASKAZINI
AFISA PSPF IRINGA AKIONGEA NA BAADHI YA WAALIMU MUFINDI KASKAZI
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Serikali Mkoa wa Iringa Baraka Jumanne akiongea na waalimu wa Shule za Msingi tatu Mufindi kaskazini pamoja na maafisa Elimu walio hudhuria kabla ya kukabidhi madawati Mnyalu.
Saturday, 3 May 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)









