Wednesday 8 January 2014

UZINDUZI WA MICHEZO NA ELIMU YA STADI ZA MAISHA KATA YA IKWEHA MUFINDI KASKAZINI



 Mh Mahammoudu Mgimwa akimkabidhi nahodha wa timu ya kijiji cha Ikweha Baraka Ruhanzo
Mpila kwa ajili ya mazoezi kujiandaa na mashindano.
 Mh Mahammoudu Mgimwa akizindua mashindano ya Mgimwa Cup kwa kupiga Danadana
 kabla ya Mchezo.
Timu zilizo fungua mashindano zikisalimia mashabiki waliofika kabla ya Mpambano.
Picha na Mnyalu.


  Mashindano ya mpira wamiguu yamezinduliwa Tar 01/01/2014 na Mh Mahamudu Mgimwa Mbunge wa jimbo la Mufindi kusini katika Tarafa ya sadani kata ya Ikweha  kijiji cha Ugenza.
Mashindano hayo yameanzishwa na kusimamiwa na shirika la Mgimwa foundation pamoja na umoja wawanafunzi walio maliza vyuovikuu wilayani mufindi (MUYOWIRUDE)
Akiohutubia wananchi wa kata ya Ikweha pamoja na wanamichezo waliohudhuria katika kiwanja cha Shule yamsingi katanihapo kabla ya uzinduzi.
 Mh Mgimwa alisema nidhamira yake na viongozi anaoshirikiana nao kuhakikisha vijana katika jimbo lake wananufaika kwa kupitia michezo nahasa kwa msimu huu kaanza na kata ya Ikweha
Mashindano hayo yatajumuisha timu tano za kata hiyo nazo ni kutoka katika vijiji vya Ikweha,Ugenza,Ilangamoto, Sinai pamoja na Ukeremi.
Akizungumzia zawadi Mh mgimwa alisema Mshindi wa kwa nza atapata jumla ya Track suti 16 zenye thamani ya shiringi 480,000/=pamoja na mipira miwili yenye thamani ya shilingi 150,000/= jumla yake ni Tshs. 630,000/=
Mshindi wa pili atazawadiwa seti ya Jezi yenye thamani ya shilingi 150,000/=pamoja na mipira miwili ya Shilingi 150,000/= jumla yake ni Shilingi 300,000/=
Mshindi wa tatu atapata mipira miwili yenye thamani ya shilingi 150,000/= awali Mh mbunge Mahamodu Mgimwa alitoa seti ya Jezi katika kila timu pamo na mpira mmoja wa mazoezi.
Pia alikabidhi mipira miwili kwa waamuzi wa mashindanohayo kwaajili ya kushindania sambamba na hilo Mh mgimwa atatoa zawadi zifuatazo.
  Mfungaji wa goli la kwanza katika mashindano hayo atapata shilingi 20,000/=,Mchezaji mwenye nidhamu atapata shilingi 30,000/= pia timu yenyenidhamu itapata shilingi 50,000/= na Mchezaji bora atapata shilingi 50,000/=
Akiwaasa vijana kwa kupitia mashindano hayo Mh Mgimwa alisema vijana wawewasikivi watakapo kuwa wakipatiwa mafunzo ya stadi za maisha kwakupitia wawezeshaji toka shirika la (MUYOWIRUDE).
Ambao wataenda sambamba na michezo hiyo kwani watapa kujifunza bure aliwaomba wajitokeze kwa wingi.
Nae Marko Shayo kiongozi wa NG’OS (MUYOWIRUDE) alisema wao watatoa elimu yanamna yakujikinga na maambukizi ya Ukimwi,Elimu ya Ujasiriamali kwakutumia
Rasilimali zinazo wazunguka katika mazingira yao hukohuko vijijini pia elimu ya jinsia na unyanyapaa katika jamii.
Akizungumza na mwandishi Nd,Albrto Chaula mkazi wa kata ya Ikweha alisema wamepokea kwafuraha mashindano hayo yatakayoenda sambamba na upataji waelimu ya stadi za maisha kwani waosasa jukumulao ni kujitokeza kwa wingi iliwapate faida itakayo wafaa maishani.
Mwisho.
Said Ngamilo.        

Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment