Mpila kwa ajili ya mazoezi kujiandaa na mashindano.
Mh Mahammoudu Mgimwa akizindua mashindano ya Mgimwa Cup kwa kupiga Danadana
kabla ya Mchezo.
Timu zilizo fungua mashindano zikisalimia mashabiki waliofika kabla ya Mpambano.
Picha na Mnyalu.
Mashindano ya
mpira wamiguu yamezinduliwa Tar 01/01/2014 na Mh Mahamudu Mgimwa Mbunge wa
jimbo la Mufindi kusini katika Tarafa ya sadani kata ya Ikweha kijiji cha
Ugenza.
Mashindano hayo
yameanzishwa na kusimamiwa na shirika la Mgimwa foundation pamoja na umoja
wawanafunzi walio maliza vyuovikuu wilayani mufindi (MUYOWIRUDE)
Akiohutubia
wananchi wa kata ya Ikweha pamoja na wanamichezo waliohudhuria katika kiwanja
cha Shule yamsingi katanihapo kabla ya uzinduzi.
Mh Mgimwa
alisema nidhamira yake na viongozi anaoshirikiana nao kuhakikisha vijana katika
jimbo lake wananufaika kwa kupitia michezo nahasa kwa msimu huu kaanza na kata
ya Ikweha
Mashindano hayo
yatajumuisha timu tano za kata hiyo nazo ni kutoka katika vijiji vya
Ikweha,Ugenza,Ilangamoto, Sinai pamoja na Ukeremi.
Akizungumzia
zawadi Mh mgimwa alisema Mshindi wa kwa nza atapata jumla ya Track suti 16
zenye thamani ya shiringi 480,000/=pamoja na mipira miwili yenye thamani ya
shilingi 150,000/= jumla yake ni Tshs. 630,000/=
Mshindi wa pili
atazawadiwa seti ya Jezi yenye thamani ya shilingi 150,000/=pamoja na mipira
miwili ya Shilingi 150,000/= jumla yake ni Shilingi 300,000/=
Mshindi wa tatu
atapata mipira miwili yenye thamani ya shilingi 150,000/= awali Mh mbunge
Mahamodu Mgimwa alitoa seti ya Jezi katika kila timu pamo na mpira mmoja wa
mazoezi.
Pia alikabidhi
mipira miwili kwa waamuzi wa mashindanohayo kwaajili ya kushindania sambamba na
hilo Mh mgimwa atatoa zawadi zifuatazo.
Mfungaji
wa goli la kwanza katika mashindano hayo atapata shilingi 20,000/=,Mchezaji
mwenye nidhamu atapata shilingi 30,000/= pia timu yenyenidhamu itapata shilingi
50,000/= na Mchezaji bora atapata shilingi 50,000/=
Akiwaasa vijana
kwa kupitia mashindano hayo Mh Mgimwa alisema vijana wawewasikivi watakapo kuwa
wakipatiwa mafunzo ya stadi za maisha kwakupitia wawezeshaji toka shirika la
(MUYOWIRUDE).
Ambao wataenda
sambamba na michezo hiyo kwani watapa kujifunza bure aliwaomba wajitokeze kwa
wingi.
Nae Marko Shayo
kiongozi wa NG’OS (MUYOWIRUDE) alisema wao watatoa elimu yanamna yakujikinga na
maambukizi ya Ukimwi,Elimu ya Ujasiriamali kwakutumia
Rasilimali zinazo
wazunguka katika mazingira yao hukohuko vijijini pia elimu ya jinsia na
unyanyapaa katika jamii.
Akizungumza na
mwandishi Nd,Albrto Chaula mkazi wa kata ya Ikweha alisema wamepokea kwafuraha
mashindano hayo yatakayoenda sambamba na upataji waelimu ya stadi za maisha
kwani waosasa jukumulao ni kujitokeza kwa wingi iliwapate faida itakayo wafaa
maishani.
Mwisho.
Said Ngamilo.
No comments:
Post a Comment