Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Tuesday, 2 June 2015
Thursday, 2 April 2015
Wednesday, 19 February 2014
Saturday, 15 February 2014
Rais Kikwete: Kuna majangili papa 40 nchini
Habari Kuu
Posted 5 hours ago
>Wakati kuna joto la vyombo vya habari vya kimataifa kuituhumu
Tanzania kuwa haipambani na ujangili, Rais Jakaya Kikwete amesema
Serikali imeubaini mtandao unaojumuisha watu 40, akiwemo tajiri maarufu
mkoani Arusha....Chanzo Mwananchi
Mnyalu.
Yanga yatisha, Komorozine wakubali kufa
Wachezaji wa Yanga wakijianda kwa mazoezi kwenye Uwanja wa Mitsamiouli mjini Moroni, Comoro
Chanzo mwanaspot..
Thursday, 13 February 2014
Amuua mwenzake wakigombea sigara
Tanga. Uvutaji wa sigara umeleta maafa, baada ya mtu mmoja kukatwa mkono na kuuawa na mwenzake wakati wakigombea sigara.
Katika tukio hilo lililotokea Korogwe, Jumapili iliyopita, Februari
2, mnamo saa nne asubuhi, Idi Mkono, mwenye umri wa miaka 30 alimkata
mkono Ramadhani Gudelo (35) na kumuua baada ya kutokea ugomvi uliohusu
sigara.Kamanda Massawe ameitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, badala yake wafuate taratibu na sheria zilizopo.
Wakati huo huo, watu wawili wanashikiliwa na polisi, mkoani hapa kwa tuhuma za kukamatwa na lita 147 za pombe haramu ya gongo maeneo ya Handeni, mkoani Tanga.
Kamanda Massawe alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa watuhumiwa hao lilitokea Februari 2 mwaka huu saa 5:30 asubuhi.
Massawe aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hussen Muhadu (48), pamoja na Ramadhani Ugarawe (40), wote wakazi wa Chanika Handeni.
Alisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Aidha Kamanda Massawe aliwaonya wananchi kuchukua tahadhari na matendo ya uhalifu wa aina yoyote ambao unaweza kusababisha kuvunja sheria, huku akionya kuwa kwa yeyote atakayekiuka sheria zilizowekwa atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.
CHANZO:MWANANCHI
KESI YA MAUAJI YA MWANGOSI YAANZA KUSIKILIZWA
Na: BerdinaMajinge,Iringa
MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa imeanza kusikiliza kesi ya muuaji wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha channel ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi huku vituko na visa baina ya wanahabari na askari wa jeshi la polisi mkoani Iringa vikiendelea kuchukua sura mpya hali inaleta maswali miongoni mwa wafuatiliaji wa kesi hiyo.
MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa imeanza kusikiliza kesi ya muuaji wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha channel ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi huku vituko na visa baina ya wanahabari na askari wa jeshi la polisi mkoani Iringa vikiendelea kuchukua sura mpya hali inaleta maswali miongoni mwa wafuatiliaji wa kesi hiyo.
katika kesi hiyo wakili wa serikali Adolph Maganda amedai
mahakamani hapo mbele ya Jaji Mary Shangali kuwa mnamo tarehe 2 septemba mwaka
2012 askari no g. 2573 wa jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia mkoani
Iringa Pasificus Ceophace simon alimuua Daudi Mwangosi kwakukusudia kinyume na
kifungu cha kanuni ya adhabu no 196 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho
mwaka 2002
Wakili huyo wa serikali amewasilisha mahakamani hapo vielelezo vya
ushahidi wa kesi hiyo ikiwemo ripoti ya kitabibu iliyotolewa na mganga
aliyefanyia uchunguzi mwili wa marehemu mwangosi, kitabu cha kumbukumbu za kutoa
na kurudisha silaha kituoni, ripoti ya mtaalam wa milipuko, mahojiano ya ungamo
na onyo pamoja na gazeti la mwananchi la tarehe 3 septemba 2012 lenye picha ya
mtuhumiwa akiwa ameshikilia silaha aliyoitumia kumfyatulia marehemu
Hata hivyo mtuhumiwa licha ya kukiri kuwepo katika eneo la nyololo
wilayani mufindi siku hiyo ya tukio amekana shitaka hilo na kesi hiyo
imeahirishwa mpaka hapo itakapopangiwa siku ya kusikilizwa tena na mtuhumiwa
amerudishwa rumande
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mwandishi wa habari wa magazeti
ya Dairy News na Habari leo mkoani iringa Frank Leonard alikamatwa na polisi
kwa tuhuma za kupiga picha wakati mahakama ikiendelea ambapo alishikiliwa
kwamuda na baadae kufikishwa katika kituo cha polisi iringa kabla ya kuachiwa
bila kuandika maelezo.
mwisho
MWENYEKITI IRINGA PRESS CLUB AKAMATWA NA KUACHIWA
Frenck Leonard akiongea na waandishi baada ya kuachiwa na Polisi alipo kamatwa ndani ya mahakama wakimtuhumu kuvunjasheria wakati akisikiliza kesi ya Mshitakiwa wa mauaji ya Daud Mwangosi aliekuwa mwandishi wa Chanel ten na Mwenyekiti wa (IPC)
Waandishi wa habari Wakiwa viwanja vya mahakama ya wilaya iringa wakisubili kupata maelezo kwa msajili wa mahakama juu ya kitendo cha Polisi kumkamata Mwennyekiti wa IPC wakimshuku kuvunja sheria ndani ya mahakama kosa ambalo halikujulikana nakupeleke kumuachia huru.
Askari kanzu wakimpa ulinzi mtakatifu mshitakiwa wa kosa la mauaji ya aliekuwa muandishi wa chanel ten Daudi Mwangosi wakati ana toka mahakamani leo kwa kumpandisha katika gari maalumu ili asipigwe picha na waandishi baada ya kesi yake kuandikishwa rasimi katika mahakama kuu na itajadililiwa katika kikao kitakacho pangwa tayali kwa kusikilizwa
Mnyalu.
Wednesday, 8 January 2014
UZINDUZI WA MICHEZO NA ELIMU YA STADI ZA MAISHA KATA YA IKWEHA MUFINDI KASKAZINI
Mh Mahammoudu Mgimwa akimkabidhi nahodha wa timu ya kijiji cha Ikweha Baraka Ruhanzo
Mpila kwa ajili ya mazoezi kujiandaa na mashindano.
Mh Mahammoudu Mgimwa akizindua mashindano ya Mgimwa Cup kwa kupiga Danadana
kabla ya Mchezo.
Timu zilizo fungua mashindano zikisalimia mashabiki waliofika kabla ya Mpambano.
Picha na Mnyalu.
Mpila kwa ajili ya mazoezi kujiandaa na mashindano.
Mh Mahammoudu Mgimwa akizindua mashindano ya Mgimwa Cup kwa kupiga Danadana
kabla ya Mchezo.
Timu zilizo fungua mashindano zikisalimia mashabiki waliofika kabla ya Mpambano.
Picha na Mnyalu.
Mashindano ya
mpira wamiguu yamezinduliwa Tar 01/01/2014 na Mh Mahamudu Mgimwa Mbunge wa
jimbo la Mufindi kusini katika Tarafa ya sadani kata ya Ikweha kijiji cha
Ugenza.
Mashindano hayo
yameanzishwa na kusimamiwa na shirika la Mgimwa foundation pamoja na umoja
wawanafunzi walio maliza vyuovikuu wilayani mufindi (MUYOWIRUDE)
Akiohutubia
wananchi wa kata ya Ikweha pamoja na wanamichezo waliohudhuria katika kiwanja
cha Shule yamsingi katanihapo kabla ya uzinduzi.
Mh Mgimwa
alisema nidhamira yake na viongozi anaoshirikiana nao kuhakikisha vijana katika
jimbo lake wananufaika kwa kupitia michezo nahasa kwa msimu huu kaanza na kata
ya Ikweha
Mashindano hayo
yatajumuisha timu tano za kata hiyo nazo ni kutoka katika vijiji vya
Ikweha,Ugenza,Ilangamoto, Sinai pamoja na Ukeremi.
Akizungumzia
zawadi Mh mgimwa alisema Mshindi wa kwa nza atapata jumla ya Track suti 16
zenye thamani ya shiringi 480,000/=pamoja na mipira miwili yenye thamani ya
shilingi 150,000/= jumla yake ni Tshs. 630,000/=
Mshindi wa pili
atazawadiwa seti ya Jezi yenye thamani ya shilingi 150,000/=pamoja na mipira
miwili ya Shilingi 150,000/= jumla yake ni Shilingi 300,000/=
Mshindi wa tatu
atapata mipira miwili yenye thamani ya shilingi 150,000/= awali Mh mbunge
Mahamodu Mgimwa alitoa seti ya Jezi katika kila timu pamo na mpira mmoja wa
mazoezi.
Pia alikabidhi
mipira miwili kwa waamuzi wa mashindanohayo kwaajili ya kushindania sambamba na
hilo Mh mgimwa atatoa zawadi zifuatazo.
Mfungaji
wa goli la kwanza katika mashindano hayo atapata shilingi 20,000/=,Mchezaji
mwenye nidhamu atapata shilingi 30,000/= pia timu yenyenidhamu itapata shilingi
50,000/= na Mchezaji bora atapata shilingi 50,000/=
Akiwaasa vijana
kwa kupitia mashindano hayo Mh Mgimwa alisema vijana wawewasikivi watakapo kuwa
wakipatiwa mafunzo ya stadi za maisha kwakupitia wawezeshaji toka shirika la
(MUYOWIRUDE).
Ambao wataenda
sambamba na michezo hiyo kwani watapa kujifunza bure aliwaomba wajitokeze kwa
wingi.
Nae Marko Shayo
kiongozi wa NG’OS (MUYOWIRUDE) alisema wao watatoa elimu yanamna yakujikinga na
maambukizi ya Ukimwi,Elimu ya Ujasiriamali kwakutumia
Rasilimali zinazo
wazunguka katika mazingira yao hukohuko vijijini pia elimu ya jinsia na
unyanyapaa katika jamii.
Akizungumza na
mwandishi Nd,Albrto Chaula mkazi wa kata ya Ikweha alisema wamepokea kwafuraha
mashindano hayo yatakayoenda sambamba na upataji waelimu ya stadi za maisha
kwani waosasa jukumulao ni kujitokeza kwa wingi iliwapate faida itakayo wafaa
maishani.
Mwisho.
Said Ngamilo.
STADI ZA MAISHA YA JAMII YETU.
Stadi za kazi kwa watoto waishio vijijini huwa ni kwa vitendo zaidi picha hizi kijijini Mtitu kata ya Mtitu Wilaya ya Kilolo.
Kilimo kwanza ni dhana inayosemekana na kufikirika ila haijatendeka ipasavyo vijijini.Wanyama kazi na changamoto zake wakati wa matumizi vijijini hapa ni kijiji cha Kitowo kata ya Mtitu Wilaya ya Kilolo.
.
Usafiri wetu.
(Picha zote na Mnyalu)
Tuesday, 7 January 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)




