Saturday 15 February 2014

JARIBU KULA PICHI UONE FAIDA ZAKE.


Tofauti na matunda mengine mapichi.yana majina mengi tofauti tofauti. Majina haya hutofautiana kulinga na maeneo yanapolimwa Watu wa Arusha huyaita Matipisi lakini wale wa Iringa wanayafahamu kama Mapindigesi Tunda hili lina kiasi kidogo sana cha lehamu, Mafuta hata sodium. Kwa kawaida matunda haya yapo ya aina mbili,yapo yale ya Njano na yale Meupe.

Vitamini.

Mapichi yana aina kumi za vitamini nazo ni pamoja na A,C,E,K, na sita za B complex. Vitamin A na beta carotene husaidia kuongeza uwezo wa macho kuona wakati vitamin C nikuondosha sumu kinachosaidia kuboresha kinga ya mwili. 

Pamoja na kuwa tunda hili lina kiasi kidogo cha vitamin E na k. Vitamin E ni kiondosha sumu kingine. Wakati vitamin K ni muhimu kataka kusaidia damu kuganda. Tunda hili pia ni chanzo kizuri cha madini thiamin, riboflavin, vitamin B-6 niacin, folate na pantothenic acid hivi ni virutubisho muhimu sana katika uboreshaji wa seli za mwili na mifumo ya fahamu.

Nyuzi nyuzi,  Faida nyingine muhimu ya Pichi ni ule uwezo wake mkubwa wa kusaidia suala zima la mmeng'enyo wa chakula Nyuzi nyuzi hizi pia husaidia kudhibiti kiwango cha lehamu mwilini na hivyo kusaidiakupunguza uwezokano wa kupata magonjwa ya moyo.

Chanzo Mwananchi.

Mnyalu. 

     


Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment