Tuesday, 13 June 2017

NAMAINGO BUSINESS AGENCY

SHEREHE

Ngoma ya Jamii ya kimasai ikitumbuiza katika sherehe ya Mahafali chuo cha Biashara iringa hivi karibuni.

ZIARA YA MKURUGENZI WA NAMAINGO IRINGA

Mkurugenzi wa Namaingo Busines Agency Tanzania katikati pichani BiUbwa Ibrahim alipo tembelea eneo la Mradi wa wanachama wa Namaingo katika kijiji cha Itagutwa hivi karibuni
Mnyalu.

Tuesday, 3 May 2016

MAJI VIJIJINI

Mmoja wa wanakijiji wa Kinyika kata ya Mlenge Tarafa ya Pawaga Wilaya ya Iringa akichota maji Kisimani kwa Matumizi ya Nyumbani. Said Ng'amilo
Rozi Mahai akimvisha Mumewe Pete ya Ndoa Tar 29-08-2014 katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa,      hivi sasa wanatarajia kufika kanisani kujikabidhi kwa Bwana kufunga ndoa ya kidini wabarikiwe sana.

Monday, 23 November 2015

TUNAFATA MAJI

Wananchi wa Kijiji cha Kinyali kata ya Migoli wakifuata Mji Bwawa la Mtera yapata umbali wa maili 3,,kwa matumizi ya kufua na kuoga.

Thursday, 29 October 2015

DK JOHNI MAGUFULI KIDEDEA URAISI

DK Johni Magufuli wa CCM aibuka kidedea uchaguzi mkuu nafasi ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata kura ....8,882,935 Votes 58.46 %.......dhidi ya Mpinzani wake Edwad Lowassa wa Chadema akipata kura 6,072,848 Votes (39.97 %, na kutangazwa mshindi, anatarajiwa kuapishwa hivikaribuni. 

RC ANENA

Mkuu wa Mkoa wa Iringa akiongea na waandishi wa Habari Manispaa ya Iringa kuhusu ujumbe wa amani baada ya Uchaguzi,kwakuwataka wananchi waheshimu maamuzi yaliotokea ili kuendelea na kazi za Maendeleo,

Wednesday, 28 October 2015

SHANGWE, HOIHOI, VIFIJOOOOOOOOOO.

Wapenzi na wanachama wa Chadema wakishangilia nje ya ofisi za Manispaa wakisubiri matokeo ya Ubunge Jimbo la Iringa Mjini juzi.

SALAMU KWA WANANCHI MAMBOOOOOOOOO

Mh Peter Msigwa akisalimia wananchi wamanispaa Iringa kwa kupunga mkonowakati wakisubiri kutangazwa matokeo kushoto ni Mzee mwanamageuzi mkongwe Iringa Butinini.

MCH PETER MSIGWA ATANGAZWA MBUNGE.

Mh Peter Msigwa akiwaasa wananchi wa Manispaa ya Iringa kuwa watulivu wakati wakisubiri matokeo juzi. kushoto ni Msimamaizi wa uchaguzi Jimbo la Iringa Ahmad Sawa.

Tuesday, 27 October 2015

CHADEMA WASHEREHEKEA USHINDI

Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, wakiweka Bendera eneo la Ofisi ya Kampeni za Uchaguzi 2015, oktoba,25 baada ya kupata dalili za Ushindi tar 26 asubuhi.

Friday, 23 October 2015

MKUTANO WA KAMPENI CCM

Add caption
Washabiki wa ccm wakiwa katika mfanano wa rangi za chamachao katika mkutano wa kampeni ya mgombea Urais kupitia ccm,

Sunday, 18 October 2015

MATUKIO MSIBA WA DEO FILIKUNJOMBE

Mjane wa Marehemu anaepunga mkono pichani akiashiria huzuni na kuaga.

 Spika wa Bunge Anna Mkinda akisalimiana na kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo Zitto kabwe

 Ris Jakaya kikwete akipita kuwapa mkono wa fiwa wakati wa kuaga mwili wa Deo na wenzake Lugalo Hospitali
Picha Nyumani kwa marehemu Deo Filikunjombe Mtoni kijichi Dar es salaam.

NI MSIBA WA TAIFA

JK aongoza mamia ya watanzania kuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Ludewa na wenzake wawili katika hospitali ya Jeshi Lugalo kabla ya kuanza safari kuelekea Njombe, Ludewa kwa Mazishi.
angalia matukio katika picha Mnyalu1blogspot.com

Thursday, 15 October 2015

WAMESAINI MKATABA.



Barozi wa Japani nchini Masaharu Yoshida na Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Muhandisi, Patrick Mfugale wakitia saini mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Juu (FLYOVR) ya makutano ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara, katika hafla iliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Picha na Said Ng’amilo 

Wednesday, 14 October 2015

KIWANDA KIPYA CHA SARUJI

Sehemu ya kiwanda kipya cha Saruji Mtwara.

KIWANDA CHA ZAMANI CHA SARUJI.

Kiwanda cha Saruji cha zamani kilichopo Mtwara, Mahala ambapo kimejengwa kiwanda cha Muwekezaji 
Aliko Dangote (DANGOTE SIMENTI). Picha na Said Ng'amilo

SEHEMU YA KIWANDA CHA DANGOTE SIMENTI MTWARA.

Picha sehemu ya Ofisi na Sehemu Kiwanda cha Saruji Dangote simenti.Mtwara.

JK AWEKA JIWE LA MSINGI NHC MTWARA

Rais Jakaya Kikwete akiweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba za makazi na Biashara zinazo jengwa na Shirika la Nyumba Mtwara, kushoto ni Mkurugenzi mkuu NHC  Nehemia Mchechu na kulia ni Mgombea Ubunge Mtwara mjini. Picha na Said Ng'amilo