Monday, 20 January 2014

MBUNGE WA IRINGA MJINI AMTAKA KATIBU WA CCM KUACHA KUPOTOSHA UMMA



Mch Peter Msigwa Mbunge Iringa mjini akiongea na wananchi wa manispaa ya Iringa hivi karibuni katika viwanja vya Mwembetogwa.
Mnyalu.

Iringa
MBUNGE wa iringa mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo
(chadema) mchungaji Peter Msigwa amemtaka katibu wa ccm wilaya ya
iringa kuacha kupotosha umma kuhusiana na kiasi cha fedha zinazotolewa
kwa ajili ya maendeleo ya jimbo kiasi cha shilingi milioni30 kwa
mwaka.

Msigwa ametoa rai hiyo kufuatia taarifa iliyotolewa juzi na katibu wa
ccm wilaya ya iringa Hassan Mtenga siku tatu zilizopita ambapo katibu
huyo alisema kuwa mbunge huyo analetewa kiasi cha shilingi milioni 15
kwa mwezi na hivyo kumuagiza meya wa manispaa ya iringa Aman Mwamwindi
kumuhoji mbunge huyo kuhusiana na matumizi ya fedha hizo.

Msingwa  Alisema  kuwa fedha hizo zimeshapelekwa katika baadhi ya miradi ya
maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari ya katika kata ya nduli
inayotarajiwa kukamilika kuanzia machi mwaka huu na kwamba yeye hawezi
kuzitumia kwa matumizi yake binafsi kwasababu kwanza fedha hizo
huingizwa moja kwa moja katika akaunti ya halmashauri katika jimbo
husika na mbunge wa jimbo anabakia kuwa ndiye mwenyekiti wa mfuko
akisaidiwa na wajumbe kutoka katika vyama vyote hivyo lengo la katibu
huyo wa ccm ni kutaka kunichafua kisiasa.

“Siamini kuwa katibu huyo hajui kiasi cha fedha zinazotolewa kwaajili
ya mfuko wa jimbo ila yeye ametaka kunichafua mimi kisiasa na
kuudanganya umma na wana iringa ili waone kwamba mbunge wao hafai”
alisema msigwa.
Msigwa alisema hayo jana wakati akiwahutubia wananchi wa kata ya nduli
katika uzinduzi kampeni katika uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye kata
hiyo iliyopo manispaa ya iringa.

Alisema kuwa kuwa mtenga asitegemee kubadilisha chochote kwenye
siasaza iringa mjini kwani wananchi walishaipa madaraka ccm ikashindwa
kuwaletea maendeleo hivyo hawana tena sababu ya kukiamini chama hicho
katika nafasi yoyote ya uongozi

Nae mgombea  udiwani kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo
Chadema  katika kata  hiyo Ayub Mwenda  ambae  pia aliwahi kuwa
mwenyekiti wa kijiji  cha Nduli,aliwaomba wananchi wa kijiji hicho
kumchagua ili aendelee kupigania maendeleo ya kata hiyo akisaidiana na
mbunge msigwa.

Vyama viwili vya siasa CCM  na CHADEMA ndiyo pekee wanaoshiriki katika
uchaguzi huo mdogo katika kata ya Nduli mkoani Iringa.

Uchaguzi  huo umekuja  kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo
marehemu Idd Chonanga kufariki dunia Julai nne     mwaka jana.
MWISHO.
Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment