Msaidizi
wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayeshughulikia maswala ya haki za binadam,
Ivan Simonovic, ameiambia BBC kuwa pande mbili zilizo kwenye mgogoro nchini
Sudan Kusini zimehusika katika utekelezaji wa vitendo vya mauaji.
Bwana
Simonovic amekuwa kwenye ziara ya maeneo mbalimbali ya Sudan Kusini ili kupata
ukweli kwa ajili ya kuandaa ripoti ya Umoja wa Matifa na ameelezea kuwa ana
ushahidi wa kutosha kusema pande mbili kwenye mgogoro zina hatia.
Taarifa zinazohusiana
Ripoti
hiyo pindi itakapokuwa tayari, ataiwasilisha kwa Baraza la usalama la umoja wa
mataifa, hasa kutathimini mauaji yaliyojitokeza katika mgogoro ulioanza mwezi
Disemba mwaka jana.
Maelfu
ya watu wameuawa katika mwezi mmoja uliopita katika mgogoro kati ya serikali na
waasi wanaoongozwa na makamu wa zamani wa Rais Riek Machar.
Bwana
Simonovic aliambia BBC kwamba pande zote mbili serikali na waasi zilifanya
uhalifu.
"Lakini
kila upande ulihusika kwa kiwango fulani na katika maeneo tofauti. ''
Simonovic
amesema kuwa maeneo yaliyoathirika zaidi, yalikuwa Mji wa Bor kusini mwa nchi
hiyo na Bentiu Kaskazini mwa nchi hiyo.
Wiki
jana watu 200 walikufa maji katika ajali ya boti walipokuwa wanakimbia vita
"Mji
wa Bor hauna watu na Bentiu umekuwa kama mji ambao haujawahi kuishi watu.
Haujaporwa bali umeteketezwa, '' alisema bwana Simonovic.
"Raia
wapo kwenye kambi za wakimbizi wa ndani.Kinachochukiza ni kwamba kuna tatizo la
ukabila hapa ambavyo mgogoro ulianza na nani anayewalenga raia.''
"Nadhani
ni muhimu kuweza kuchunguza kwa undani chanzo cha mgogoro na pia kuripoti
unyama unaotendewa raia.''
Bwana
Simonovic amesema ripoti yake itakuwa tayari katika wiki chache zijazo.
Mgogoro
huu ulizuka Disemba tarehe 15 wakati ambapo Rais Salva Kiir alimtuhumu
aliyekuwa makamu wake wa Rais Riek Machar kwa kupanga njama ya mapinduzi dhidi
ya serikali yake.
Chanzo BBC,
No comments:
Post a Comment