Ndugu zangu,
Matayarisho yanaendelea kabla ya uzinduzi rasmi wa matangazo ya mtandaoni ya Redio ya Kwanza Jamii itakayokuwa ikitangazia kutoka Akiba House, Iringa.
Kama ilivyo jina lake, Kwanza Jamii Redio ni Redio ya Kijamii yenye kumweka mwanajamii KWANZA. Jiandae kusikiliza Redio ya tofauti. Itakuwa pia ikipatikana hewani kwa baadhi ya vipindi kupitia Redio ya Kijamii ya Nuru FM ya hapa Iringa.
Tunataraji ushirikiano wako katika kufanikisha kazi yetu hii ya kuitumikia jamii.
Taratibu Tunasonga Mbele...
Maggid Mjengwa,
Iringa.(Mjengwablog chano)
No comments:
Post a Comment