Monday 24 February 2014

matokeo ya mechi kati ya Lipuli Sc na Kimondo FC ya Mbalizi Mbeya


 Mwamuzi wa mpira wa Lipuli sc na Kimondo Fc Krina Kabara akitolewa nje kukwepa ugonvi uliokuwa unaendelea uwanjani hapo baada ya mpira kumalizika...

Iringa.
MWAMUZI  wa mpira  kati ya Lipuli Sc ya mjini Iringa na Kimondo Fc  ya Mbalizi Mbeya Krina Kabara uliochezwa jana katika kiwanja cha Samora na kutoka sare ya goli moja anusulika kupigwa kwa madai ya kupendelea timu moja na kuisababishia Lipuli isipande daraja.

Mashindano hayo ya  ligi daraja la kwanza ambayo yanaendelea yalisababisha muamuzi huyo kushambuliwa kitendo kilicho sababisha mashabiki pamoja na baadhi ya wachezaji kumshutumu  mwamuzi huyo kuwa amechezesha mchezo huo kwa matakwa ya mwenyekiti wa Lipuli.

Lipuli sc ilijipatia goli la kwanza kunako dakika ya 3 ambalo lilifungwa na Abdala Matimila katika kipindi cha kwanza na BarakaMtafya wa Kimondo Fc aliifungia timu yake kwa penati kusawazisha goli hilo dakika ya 9 .

Akizungumza mwenyekiti wa Lipuli Sc Abuu Chang’aa alisema kuwa tuhuma za kuwa kauza mechi kwa  kuwapa wachezaji wa Lipuli fedha ili wacheze chini yakiwango si  kweli kwasababu anapenda maendeleo ya timu hiyo na anataka izidi kusonga mbele zaidi.

“Mimi siwezi kuwalipa wachezaji ili wacheze chini ya kiwango pesa nilizo wapa ni kwa ajiri ya usajiri wengine hawakuwa wamemaliziwa kulipwa,kama hawawezi na hawana imani na timu yao waache kuchezea”alisema Abuu

Abuu aliongeza kuwa mechi ijayo Lipuli inatarajia kucheza na timu ya Majimaji Fc na Mlale ya mjini songea ambapo wataondoka alihamis wiki hii kuelekea Songea kwamichezo hiyo ambapo Lipuli inapointi 14 na kimondo inapointi 11.

MWISHO.


Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment