Wednesday, 19 February 2014

MGOMBEA UBUNGE KALENGA CCM AWEKEWA PINGAMIZI.







Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa Iringa  (CHADEMA) Pamoja na mgombea ubunge kalenga Grace Tendega kimewasilisha fomu ya pingamizi kwa mgombea ubunge ccm jimbo la kalenga Ndg Godfrey Mgimwa kwa Msimamizi wa uchaguzi wilaya Iringa.
 viongzi wa Chadema Mkoa na Wilaya waliwasiri katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi kusikiliza pingamizi lao na hatimae muda wa saa 10:00 ulipowadia  hakukuwa na tangazo kwa wagombea walio ludisha fomu kuruhusiwa kwenda kuendelea na kampeni.

 Mh Nyalusi Diwani chadema kata ya Mivinjeni manispaa ya Iringa alisema wanaenda kuandika barua kuthibitisha pingamizi lao na kuiwasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
Wagombea walio ludisha fomu za ugombea Godfrey Mgimwa ccm,Grace Tendega Chadema, na Richardi Minja Chausta. Mgombea kutoka NCCR MAGEUZI Erick Chelula  alichelewa kulejesha fomu na ameondolewa katika kinyang'anyilo hicho.
Mnyalu,
Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment