Mshambuliaji wa timu ya yanga, Mrisho
Ngasa (17) akichuana vikali ili kuwania mpira na beki hodari wa timu ya
Mbeya City, Deogratias Julius kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara
ambapo timu ya Yanga iliibuka na ushindi kwa kuichapa timu ya Mbeya
city goli 1-0, goli la Yanga lilipachikwa na Mrisho Ngasa mnamo dakika
ya 15 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Beki wa timu ya Mbeya City, Deogratias Julius akiondoa mpira katika eneo la hatari kwenye lango la timu hiyo.
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haroun Niyonzima pamoja na beki wa Mbeya City, Yussuf Abdallah wakichuana vikali kuwania mpira katika mchezo huo wa mzungunguko wa raundi ya pili ya ligi kuu ya Tanzania bara uliochezwa leo katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa timu ya Mbeya City wakiwa wamefurika uwanjani hapo kuishangilia timu yao.
Mbuyu Twite wa timu ya Yanga akichomoka na mpira na kumwacha mchezaji wa Mbeya City katika mchezo huo.
Hii ndiyo ilikuwa furaha ya wachezaji wa Yanga baada ya kupata goli la kwanza.na Mjengwablog.
No comments:
Post a Comment