Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Evarista kalalu akikabidhi Kompyuta mbili Paulo Mahimbi Mw /Mkuu shule ya Msingi Ugesa moja kati ya Kompyuta 5 zilizo tolewa na Mh Mahammod Mgimwa. Mnyalu.
Iringa.Halimashauri ya wilaya ya mufindi inakabiliwa na
upungufu wa madawati 4269 kwa uwiano wa dawati moja kwa wanafunzi wawili wakati
awali wilaya hiyo ilikuwa ikisifika kwa utumiaji wa madawati ya Adobe licha
ya wilaya hiyo kuvuna mbao.
Hayo yalibainishwa juzi wakati wakipokea madawati 100 na kompyuta 5 zenye thamani ya shilingi
mil 12 kutoka kwa Naibu waziri wa maliasili na utalii Mh Mohamud Mgimwa ambaye
pia ni mbunge wa jimbo la mufindi kasikazini kwa kushirikiana na mfuko wa
penseni kwa watumishi wa uma(PSPF) Iringa.
Mgeni rasimi
katika makabidhiano hayo mkuu wa wilaya ya mufindi Evarista Kalalu alisema kuwa
wilaya ya Mufindi haina upungufu wa madawati kwa uwiano wa dawati moja kwa
wanafunzi wawili upungufu uliopo niwa walimu wa sayansi kitendo kinacho
sababisha kutokuanya vizuri katika somo hilo.
“Wakuu wa shule kwa kuwa mufindi haina upungufu wa
madawati upungufu uliopo ni wa walimu wa sayansi hivyo nawaombeni masomo
yaliyosalia yaweze kuleta matokeo mazuri shuleni”alisema Kalalu
Kwa upande wake Afisa elimu msingi Mufindi Farida
Mwasumilwe alisema kuwa wanashukuru kupokea vifaa hivyo kwa sababu wanahitaji
kuboresha ili uwiano uwe kwa dawati moja kwa mwanafunzi mmoja ili waweze
kujitegemea katika mtihani wa mwisho.
“Nawashukuru wadau mbali mbali ambao wanajitokeza
katika kuweka nguvu katika sekta ya elimu na madawati haya yanaenda katika
shule ya msingi mjimwema,Mamba,
nyamalala na kompyuta zinaenda
shule za msingi Ugesa, Itona na
Igombavanu sekondali.”alisema Farida
Naye Baraka Jumanne Ofisa mfawidhi mkuu wa PSPF Iringa aliwataka walimu hao pamoja na
wanafunzi kuvitunza vifaa hivyo ili vidumu na vitumike kwa wanafunzi wengine
wanaotarajiwa kuanza masomo.
Mnyalu.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment