WANAO MILIKI SIRAHA KINYUME CHA SHERIA WATAKIWA KUZISALIMISHA HARAKA.
Mkuu wa wilaya Iringa Dr Leticia Warioba awataka wananchi wa Halmashauri ya
Iringa wanao miliki siraha kinyume cha sheria kuzisalimisha haraka iwezekanavyo
kuanzia Tar 30-12-2014 mpaka tar 01-02-2015 bila shuruti yeyote atakae
fanikisha zoezi hilo hatachukuliwa hatuazozote dhidi yake.
Akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake majira ya Saa
nane Mchana Dr Leticia Warioba alisema anawaomba wananchi watoe ushirikiano
kufanikishahilo kwani yeye na kamatiyake ya Ulinzi Kiwilaya wameazimia kuhakikisha
wanapambana vilivyo na mautukio ya
Uvunjifu wa amani na Ujangili wa Tembo katika Hifadhi za Ruaha.
Akifafanua zaidi alisema Siraha zisalimishwe katika Ofisi za
watendaji Miji/viijiji au ofisi za watendaji kata na Vituo vya Polisi vilivyo
jirani na wananchi. Sambamba na hilo aliwataka viongozi wahusika kutoa
ushirikiano wa dhati katika zoezihilo huku akibainisha kuwa baada ya tarehe
1-02-2015 kupita Msakomkari utapita Nyumba kwa Nyumba na atakae bainika kukutwa
na Siraha hatua kari dhidi yake zitachukuliwa kwa kufikishwa katika vyombo vya
Sheria.
Pia aliwatakia wananchi wa Wilaya ya Iringa na Vitongoji
vyake Heri ya Mwaka Mpya na kusherehekea kwa amani na utulivu ilikuingia mwaka
mpya wa 2015 kwa utulivu huku
akikumbusha dhana ya ulinzi shirikishi iendelee kufanyakazi katika jamii ili kudumisha amani.
Said Ng’amilo Iringa.
No comments:
Post a Comment