Monday, 15 June 2015

MALIKI MARUPU AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI DODOMA


 Uraisi Maliki Marupu akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa halmashauri kuu ya ccm mjini Dodoma baada ya kuchukua fomu za kutafuta wadhamini mikoa kuminatano Tanzania wasiopungua mianne.Mnyalu.


MALIKI MARUPU HOTUBA
Nimechukua fomu ya kugombea nafasi ya urais kutokana na changamoto muhimu
sana zinazolikabili Taifa letu..Serikali yoyote ile duniani ili iweze kutekeleza majukumu
yake kitaifa sharti iwe na baraza imara la mawaziri Ninawahaidi watanzania kuwa
nitatangaza rasimu ya baraza la mawaziri wakati nalejesha fomu yangu ya Urais ili
kutoa fursa kwa wananchi kutasmini kwa kina mienendo na uadilifu  wa Mawaziri
watakao kwenda kufanya kazi na serikali ya awamu ya tano.
Hii ni shahiri dhahili tumeona kundi kubwa la mawaziri wa kinadi mbinu na kuainisha
madhaifu ya serikali ya wamu ya nne wakati mawaziri hao walikuwa sehemu ya
uwajibikaji huo.Japo wapo mawaziri walioweza kutimiza ahadi zao na kuwa watendaji
wazuri ni mawaziri wachache sana walokuwa wawajibikaji.Mawaziri wapya
wanatarajiwa kuwa 95.4% wakati mawaziri wa zamani watakuwa 4.6% tu
Ili kusaidia sheria ya maadili ya viongozi wa umma sheria namba 13 ya 1995 kuweka
bayana rasimu ya baraza la mawaziri itakuwa nguzo muhimu ya kujenga ushirikishaji
wa umma katika kulinda na kuheshimu misingi ya uadilifu katika utumishi wa umma.
Jambo la pili natoa wito kwa umma kwamba kumekuwa nadhana kuwa watu
wanaochukua fomu za uraisi watapata nafasi za uteuzi toka kwa rais atakaechaguliwa.
Hii ni dhana potofu sana katika siasa za ujenzi wa Taifa. Nafasi za uteuzi katika serikali
ya awamu ya tano hazitatolewa kama fadhila misingi ya uwajibikaji uadilifu na haki
itazingatiwa si jambo jema hata kidiogo kuona watu wakiamini kuwa uteuzi wa nafasi
utazingatia nani aligombea nini. Lazima niunde serikali huru na yenye mitazamo tofauti
Jambo linguine ni mtazamo juu ya wagombea kunadi vipaumbele vyao ambavyo
vinaweza tofautiana na ilani ya CCM. Wagombea wengi wamekuwa wakibezwa kwa
kutoa vipaumbele vyao. Huu ni ukweli usiofichika kuwa Mh. Rais ni chanzo cha sera ya
Umma ( Source of public Policy) kwa hiyo kutoa ueledi wa kujua ukibwa wa matatizo
katika sekta ya afya, kilimo, elimu na maji ni kiashiria cha kuonyesha wananchi sifa na
vigezo vya kumchagua mtu kuwa rais atakaetokana na CCM. Na ilani ya CCM haiwezi
kushindwa kuanisha masuala muhimu yanayoisumbua nchi yetu ikiwa ni pamoja na
elimu, kilimo na michezo na Afya.Japo kunauwezekano mkubwa wagombea kuanza
kuinadi Ilani ya CCM kabla ya kuziduliwa kwa wajumbe walioandaa ilani ya CCM ndio
hao hao ni wagombea hivyo kunadalili za kuinadi Ilani kabla ya wakati
Tanzania ni tofauti na Taifa kama marekani ambao wao wanasera za Taifa na kila
chama kinatoa mbinu namna ya kuitekeleza sera ya kitaifa ila Tanzania kila mgombea
anatoa mkakati mbadala kwa utekelezaji wa sera zilizo katika ilani ya CCM
Kuzipa uwezo taasisi za serikali katika kuwajibika ipasavyo taasi ambazo
msingi wake ukiimalishwa vyema itakuwa chachu muhimu sana kiutendaji mfano wa

taasisi hizo ni kama TAKUKURU, TRA, na Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa
umma. Vyombo hivi havijapewa mamlaka kamili ya kisheria katika kutimiza majukumu
yao kikamilifu.
Kwa kiasi kikubwa TRA wamekuwa wakikutana na vikwazo vikubwa katika
ukusanyanyi wa kodi kutokana na mgongano wa kimaslahi kati ya taasisi na baadhi ya
viongozi wa umma wanaomiliki makampuni yao kibiashara wanakwepa kulipa kodi
kupitia mamlaka waliokuwa nayo hali hii inalighalimu Taifa kukosa mapato makubwa
nitahakikisha naweka mikakati makini kuhakikisha tunaongeza pato la ndani pitia
mapato ya ulipaji wa kodi na tutaboresha zaidi sheria za kodi na hatua kali kuchukuliwa
dhidi ya wakwepa kulipa kodi.
Pia TAKUKURU wamekuwa wakipata wakati ngumu katika kukabiliana na majanga ya
kuwawajibisha walarushwa kutokana na chombo hicho kukosa mamlaka kamili ya
kuwashughulikia wahujumu uchumi kisheria hili nitalishughulikia
Nafunga mjadala kuhusu umri wangu wa kugombea urais kumekuwa na
mjadala juu ya umri wangu wa ibara ya 39 (i) b na ibara 39(i) d, kuwa na mkanganyiko.
Wanasheria wengi walitoa mitazmo tofauti juu ya suala hilo ila ukirejea katiba ya
jamuhuri ya muungano ibara ya 39(i)d sifa za raisi” anazo sifa za kumwezesha kuwa
mbunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi” kifungu hiki cha kikatiba kinanipa uhuru
wa kugombea na ithibati ya hili ni kuwa kifungu hiki kimeondoloewa kabisa katika
rasimu iliyopitishwa na bunge maalumu la katiba ibara ya 88 (i) a – f
Kutokana na ukakasi wake kisheria lakini pia kifungu cha 39(i) b sifa za rais kinasema
“ametimiza umri wa mika arobaini”
Kifungu hicho kinakinzana na katiba ya nchi ibara ya 13 (2)kinasema “ ni marufuku kwa
sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika jamuhuri ya muungano kuweka
sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake “
Vilevile Tanznaia binadamu wote wanapaswa kuwa na haki ya kuchagua na
kuchaguliwa bila shuruti lolote isipokuwa mtu awe na umri wa kuanzia mika 18 kwa
mujibu wa Tangazo la haki za binadamu la mwaka 1948(30)(Unversal declaration of
human wright) lakini pia katiba inasema ibara ya 12 (i) “ binadamu wote huzaliwa huru,
na wote ni sawa” hivyo kila mmoja ni wajibu wake kuchagua na kuchaguliwa. Suala hili
la ubaguzi wa kiumri alikutananalo Mwl Nyerere tarehe 07.03.1955 alipokuwa
analihutubia baraza la udhamini la umoja wa mataifa newyork aliulizwa swali na bwana
Reid ( Newziland) kuwa Mwl alikuwa na umri mdogo hivyo alimshauri Mwl Nyerere
asubili kwanza akue ndio uendelee na harakati za kulikomboa taifa. Mwl Nyerere
alimjibu Bw Reid kuwa “ Uwezo wa mtu kiutendaji hauwezi kupimwa bila kupewa fursa
ya kutenda” ( The ability of some one to do cant be measured without having the
chance of doing) wakati huo mwl Nyere alikuwa na umri wa miaka 33 tu
Si busara kuwakashifu wagombea urais .Ni jambo la aibu sana kuona
Wanasiasa wakongwe wakiacha hoja za msingi kuhusu maendeleo ya watanzania na
kuanza kukashifiana wao kwa wao haya si maadili ya CCM wagombea wote
wanaofanya hivyo wamekiuka kanuni za uchaguzi ndani ya CCM hivyo ni wajibu wao
kufuta kauli zao za kuwabeza wagombea wenzao..Wagombea wote wanahaki sawa na
hadhi sawa ndani ya CCM
Bajeti lazima isadifu uhalisia wa mahitaji ya watanzania.Kwa kiasi kikubwa tumeona
bajeti zikisomwa katika bunge lakini wananchi hawasadifu mabadiliko ya maisha yao
kutokana na makadilio ya bajeti ya bunge hivyo nitahakikisha bajeti ya taifa inasomwa
kwa kiasi stahiki cha mapato ya ndani na si bajeti tegemezi ya fedha za wahisani
Maliki s,marupu mwanafunzi chuo kikuu cha mzumbe shahada ya
uzamili wa utawala wa umma (masters of public administration) na mwenyekiti wa
mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa morogoro(UNGO) 0712099058.

Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment