Tuesday 4 August 2015

MAGUFULI URAISI CCM ACHUKUA FOMU


 MGOMBEA kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM, John Pombe Magufuli, leo Jumanne Agosti 4, 2015, amechukua fomu za uteuzi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, tayari kwa mchakato wa kutafuta wadhamini 200 ambao ni raia wa Tanzania wenye shahada za kupigia kura. Magufuli ambaye alifuatana nna mgombea mwenza wake, Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, na viongozi na wafuasi wa CCM, alkiambiwa na maafisa wa tume hiyo nkuwa, sasa yampasa kuzunguka mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo walau miwili ya Zanzibar, ili kupata wadhamini hao na akimaliza zoezi hilo atapaswa kurejesha fomu hizo kabla ya Agosti 20, 2015.Pichani Maghufuli na mgombea mwenza wake, wakiwa kwenye gari la wazi, wakipungia mkono wananchi huku mkoba wenye fomu hizo ukiwa mbele yao. Maelfu ya wafuasi wa chama hicho, walijaa mabarabarani kuanzia barabra ya Ohio, Bibi Titi Mohammed na ile ya Lumumba, na kusababisha shughuli za kawaida kwenye maeneo hayo kusimama kwa muda ili kupisha shamrashamra hizo. Baada ya msafara ya Magufuli kutoka tume ya taifa ya uchaguzi, ulipokelewa na mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete kwenye opfisi ndogo za makao makuu hya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, ambapo Magufuli aliwaonyesa wafuasi wa CCM fomu hizo na kuwaambia sasa kazi imeanza. Magufuli anatarajiwa kupambana na mgombea wa vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa, ambaye alikihama chama hicho na kujiunga na chama kikuu cha upinzani CHADEMA, ambacho tayari kimemtangaza kuwa mgombea wake na kwa hali hiyo ndiye atakuwa mgombea wa UKAWA kutokana na makubakiano ya vyama vinavyounda umoja huo ambavyo ni CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi na NLD. Uchaguzi mkuu wa Tanzania unatarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015
Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment