MUFINDI
Shirika lisilo la kiserikali laMufindi youth and women
for rulal development (MUYOWIRUDE) kwa kushirikiana na Mgimwa Foundation limejipanga kutoa elimu ya ujasiliamali kwa vijana katika
mashindano ya ligi ya maendeleo vijijini yanayoendelea katika kijiji cha Vikula
kata ya Ihalimba ili kuondokana na adha ya ajira vijijini.
Akizungumza Mkurugenzi wa shirika Muyowirude Marco Shayo alisema kuwa
michezo hii imewakutanisha vijana wa vijiji na kata mbalimbali hivyo ni bora
kuwasaidia kwa kuwapa elimu ya ujasiliamali pamoja na kuwashauri vijana juu ua
upimaji afya zao.
Shayo alibanisha kuwa vijana hao wanajifunza jinsi ya
kutengeneza sabuni , batiki na nguo pamoja na kuwashauri kujiunga katika
vikundi vya pamoja na ili kuweza kupata mkopokwa urahisi.
“Tunatoa elimu hii kwa vijana ili waweze
kujishughulisha na sio kukaa bila kazi na hatimaye kukimbilia mjini ambapo
wataenda kupata tabu na kuishia kuwa vibaka au watoto wa mitaani”alisema Shayo
Kwa upande wao vijana hao walisema kuwa wanalishukuru
sana shirika hilo kwa kuwapatia elimu hiyo kwani wamejifunza mengi na hawaoni
sababu ya kukimbilia mjini kutokana na kwamba hata vijijini wakiwezeshwa
wanaweza kufanikiwa katika maisha.
“Tumekuwa tukikimbilia mjini kwa sababu wanasema mjini
ndio mambo yote lakini tumegundua kwamba hata vijijini pia mtu unaweza ukafanya
biashara zako na kuepuka kukimbilia mjini bila kazi ya kufanya”alisema Anania
Berdina & Mnyalu.
No comments:
Post a Comment