MUFINDI
TIMU ya mpira wa
miguu Vikula Fc imeibuka ushindi wa bao mbili kwa moja dhidi ya timu ya Nundwe Fc ambapo mashindano
hayo yalifanyika katika kijiji cha Vikula cha kata ya Ihalimba wilayani ya Mufindi.
Timu ya Vikula ilijipatia goli la kwanza kunako dakika ya 15 kupitia mchezaji wake mahili
Runy Mkiwa .
Goli la pili lilifungwa na Anania mwagama dakika ya 43
huku Muhiche akiifungia timu ya
Nundwe Fc bao moja kunako dakika ya 65.
Akizindua mashindano hayo ya ligi ya maendeleo vijijini
kata ya Ihalimba mkurugenzi wa Halimashauri ya Mufindi Peter Tweve alisema kuwa
michezo ni sehemu ya kuleta umoja na amani kwa vijana hivyo halimashauri
itaendelea kusaidiana na shirika la Muyowirude pamoja na mgimwa foundation
kuhimiza michezo vijijini kama njia ya kujifunza .
Tweve alizikabidhi timu zitakazo shiriki mashindano
hayo Jezi na mipira yenye thamani ya Tsh.1milioni timuhizo ni Nundwe, Ihalimba,
Usega, Vikula, Wamimbalwe na Ufungu secondary.
Zawadi zingine zitakazotolewa ni pamoja zawadi kwa mshindi wa kwanza jezi na mipira yenye
thamani ya shilingi laki tano,
Mshindi wa pili atazawadiwa jezi na mpira wenye thamani
ya shilling laki tatu,na mshindi wa tatu atapewa shilling laki moja na elfu
hamsini.
Mchezaji mwenye nidhamu atazawadiwa kiasi cha shilling
elfu hamsini zawadi hizo zinathamani ya shiliing million.
Fainali ya mashindano hayo yatafanyika march 13 mwaka
huu katika kijiji cha Vikula kaya ya Ihalimba wilaya ya Mufindi.
MWISHO.
Mnyalu&Berdina
No comments:
Post a Comment