Sehemu ya masalia ya bati na matandiko yalio haribiwa na mvua
SACAP Deusdedit Kamugisha Afisa wa Magereza Mkoa wa Iringa pichani kulia akiongozana na Mkuu wa gereza Pawaga SP.Sosthenes Mwakapala akikagua uharibifu ulio jitokeza katika nyumba za askari na majengo wanayo tarajia kuhamia kwamuda.
Bustani ikiwa imeharibiwa na Mvua ilionyesha ikiwa na upepo mkari
Baadhi ya Vyombo vya familia za Askari Magereza vikiwa nje baada ya Mvua kuharibu makazi yao
Nyumba kumi na tano za Askari Magereza wa Gereza Pawaga
wilaya ya Iringa zimeezuliwa na Upepo mkali ulio ambatana na mvua kubwa ya mawe
ilionyesha juzi majira ya saa 9 alasiri mpaka saa kumi na moja jioni na kuanza
tena saa mbili ya usiku mpaka saa tano usiku.
Akiongea na mwandishi wa habari Mkuu wa Gereza la Pawaga
SP.Sosthenes Mwakapala alisema adha hiyo ya mvua imesababisha familia hizo
kukosa mahala pa kuishi pamoja na thamani zilizo salia wakati walipokumbwa na mvua
hiyo ingawa hakuna madhara kwa binadamu sambamba na hilo kumeezuliwa ofisi za
tano za gereza zinazojumuisha Stoo, Bohari, Mapokezi, Utawara pia Bafu ya
wafungwa.
Madhara mengine yaliyo
jitokeza ni kuharibiwa vibaya kwa heka tano za Bustani ya gereza yenye mazao
mchanganyiko ikiwamo mashina ya Ndizi, Mipapai, Mihogo, Mahindi pamoja na Miwa
mimea hiyo imevunjika kabisa haitegemewi
kupona tena.
Mkuu wagareza la Pawaga SP. Sosthenes Mwakapala alisema wao kama
uongozi wagereza na viongozi wasaidizi wake wamechukua jukumu la kuhakikisha
askari hao na familia zao wanapata mahali pakujihifadhi kwa muda wakati
wakisubiri ufumbuzi toka ofisi ya Magereza mkoa wa Iringa. Kwakuwahamishia
katika majengo ya Shule ya Msingi, Bwalo la gereza, Ghala la chakula wakae kwa muda.
Mnyalu.
No comments:
Post a Comment