Friday, 14 February 2014

GODFREY MGIMWA ACHUKUA FOMU




DSC_0749_8cfe4.png
Mgombea ubunge katika jimbo la Kalenga kupitia chama Cha Mapinduzi Ndugu Godfrey Mgimwa amechukua fomu katika ofisi za CCM-Mkoa wa Iringa leo.
Godfrey Mgimwa amesema leo wakati akichukua fomu endapo atapewa ridhaa ya kuwatumikia wana Kalenga atahakikisha wana saidiana kutatua mambo muhimu yalio kero kwa jamii kama Maji,Zahanati na Elimu kwani ni azima yake kufanya hayo sikwakuiga bali huenda yakawa ni mambo yaliokuwa yakifanywa na Mrehemu kwaumuhimu wake.
Pia hategemei kufanya kampeni za kifahari ndani ya Jimbo la Kalenga kwani anajua nini maana ya Uchumi hasa kwahali tulio nayo tunahitaji tufanye kazi kuinua hali za wana kalenga na Tanzania kwa jumla tutasafiri kwa Gari Jimbo zima hatuta tumia Chopa 
Nae Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu alisema kampeni zitafanywa Mtaa kwa mtaa kwa kutumia mabalozi wao bilashida watashinda ingawa ni mapema kutaja ni kwa asilimia ngapi.
Godfrey Mgimwa mgombea kiti cha Ubunge jimbo la kalenga anatarajia kuludisha fomu tar 17-02-2014 saa tano as akiwa na matumaini ya kuungwa mkono kwa kudhaminiwa na wana ccm jimboni kwake.

(Picha na Mnyalu)
Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment