Monday, 17 February 2014

GRACE TENDEGA ACHUKUA FOMU YA UGOMBE UBUNGE.


Msiamazi wa Uchaguzi Pudenciana Kisaka akikabidhi fomu kwa Grace Tendega chadema mgombea ubunge jimbo la kalenga
Picha na Mnyalu.


Iringa.Mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama cha democrasia na maendeleo Chadema, Grace Tendega jana amechukua fomu ya kuwania kiti hicho huku msafara wake ukizuiwa na Polisi mkoani hapa kwa maelezo kuwa hawakuwa na kibari cha kuandamana.
Msafara wa Tendega ambao ulizuiwa na Polisi wakikuwa na siraha  jana ulianza  majira ya saa nne asubuhi katika eneo la Igumbilo umbali wa Km 7 katikati ya Mji wa Iringa.
Hadi unazuiwa tayari msafara huo uliokuwa ukiuongozwa na Pikipiki zaidi ya 50,magari zaidi ya 10 ulikuwa umetembea umbali za KM 5.5 na ulizuiwa wakati wanachama hao walipokuwa wakipandisha mlima wa Ipogolo wenye urefu wa KM 2 kutoka Ipogolo hadi ndani ya mji wa Iringa.
Namna ulivyozuiwa
Katika kile kilichotafisiliwa kama kuvurugu shamramshara zilizoandaliwa na Chadema Nyanda za juu kusini,Mkoa wa Iringa Wilaya na Jimbo, Maofisa wa Polisi waliibuka katika eneo la Mlima Ipogolo na kuzuia Pikikipiki pamoja na magari yaliyokuwa yakimsindikiza mgombea huyo kwenda kuchukua fomu huku wakiruhusu gari la Mgombea pekee kupita katika eneo hilo.
Askari hao baadhi walikuwa katika sare za Polisi na wengine kiraia huku wakiw ana siraha kitendo hicho licha ya kutafisiliwa kama kilichangia kuvurugu shamra shamra hizo pia kiliwatia hofu baadhi ya waendesha bodaboda ambao waligeuza pikipiki zao na kukimbilia mitaani.
Baada ya majadilino yaliyodumu kwa muda wa Dk 20 Ofisa wa Polisi aliruhusu gari ya Mgombea  kupita na kuelekea ziliko ofisi za tume kwa ajili ya kuchukua fumo kusisitiza kuwa asingeweza kuruhusu gari na Pikipiki kumsindikiza mgombea huyo nabadala yake akawataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kwenda kusubiri mgom bea katika ofisi za Chama hicho.
“Hapa nitaruhusu gari moja tu lililobeba mgombea ndilo litapita lakini magari mengine pamoja na Pikipiki hakuna kupita kwani kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria ninyi nendeni mkasubiri ofisini na mgombea wenu atakapochukua fomu atawakuta huko”alisema ofisa huyo wa Polisi.
 Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu,Grace aliwataka wananchi kutohofia vitendo vilivyofanywa na polisi ikiwamo ya kuzuia msafara wake bali wanapaswa kutambua kuwa huo ni mwanzo tu wa harakati za ukombozi.
Alisema chama hicho kimejipanga kupambana na kuhakikisha kinapata ushindi katika Jimbo la Kalenga na lengo kuu likiwa kuwapelekea wananchi wa Jimbo hilo ukombozi wa kweli wenye lengo la kuwapatia wananchi hao maendeleo.

“Niwaombe wakazi wa Iringa hususani wa Jimbo la Kalenga msiogope,huu ni mwanzo tu wa mapambano,siku zote haki haiombwi bali inatafutwa,nawaomba mjitokeze kwa  wingi kuunga mkono harakati hizi za ukombozi,tumieni fursa hii kuchagua  kiongozi atakayewafaa na si kuwatesa”alisema Grace.
Grace achukua fomu
Pamoja na zuio hilo lililofanywa na polisi baadhi ya wanachama wakitumia bodaboda waliwazunguka Polisi na kuwasili katika ukumbi wa siasa ni kilimo kushuhudia zoezi la uchukuaji fomu la mgombea wao.
Zoezi la uchukuaji fomu la mgom bea huyo lilifanyika majira ya saa sita mchana katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi Jimbo la KalengaPudenciana Kisaka ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halimashauri ya Iringa Vijijini.
Kisaka alimkabidhi fumo namba 8 mgombea huyo pamoja na nyaraka mbalimbali za Tume ya uchaguzi ikiwamo sheria za uchaguzi Kanuni za uchaguzi na pia katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kumtaka mgombea kwenda kujisomea kwa lengo la kuongeza uelewa ili kuepusha vurugu wakati wa kampeni na uchaguzi wenyewe.
“Paomoja na kukukabidhi fomu hii na kukabisdhi maelekezo ya vyama vya siasa na wagombea,nakukabidhi pia kanuni za wagombea mpia kipo kitabu cha sheria za vyama vya uchaguzi kanuni zimeelezwa vuzri hapa hicho kitasaidia kutogongana kisheria kitabu cha tuma nah ii katiba ya Jamuhuri ya Muugano ni vizuri ukawa nayo uipitie ili msigongane wakati w akampeni za uchaguzi”alisema Kisaka.
Kisaka aliwaambia waandishi wa habari kuwa hadi sasa ni wagombea wawili kutoka vyama vya CCM na Chadema pekee ndio wamejitokeza kuwania kiti cha Ubunge katika jimbo hilo huku akiongeza kuwa mwisho wa kurejesha fomu ni Februari 18 mwaka huu (leo).
“Hadi sasa tunavyama viwili ambavyo wagombea wake wameshachukua fomu ya kuwania Ubunge kwa jimbo la Kalenga ,hata hivyo sheria bado inatoa Fursa kwa vyama kjuendelea kujitokeza hadi kuchukua na kurejesha hadoi kesho (leo)kabla ya saa kumi jioni”alisema Kisaka.

Uchaguzi wa Kalenga unatarajia kufanyika Machi 16 mwaka huu na unalengo la kuziba pengo lililoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hil Marehemu Dk Wiliam Mfimwa aliyefariki dunia Januari Mosi mwaka huu,katika uchaguzi huo CCM imemsimamisha Godfrey Mgimwa mmoja w awatoto w amarehemu Mgimwa kupeperusha bendara ya chama hicho.
MWISHO
 

Anonymous
Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment