MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa imeanza kusikiliza kesi ya muuaji wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha channel ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi huku vituko na visa baina ya wanahabari na askari wa jeshi la polisi mkoani Iringa vikiendelea kuchukua sura mpya hali inaleta maswali miongoni mwa wafuatiliaji wa kesi hiyo.
katika kesi hiyo wakili wa serikali Adolph Maganda amedai
mahakamani hapo mbele ya Jaji Mary Shangali kuwa mnamo tarehe 2 septemba mwaka
2012 askari no g. 2573 wa jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia mkoani
Iringa Pasificus Ceophace simon alimuua Daudi Mwangosi kwakukusudia kinyume na
kifungu cha kanuni ya adhabu no 196 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho
mwaka 2002
Wakili huyo wa serikali amewasilisha mahakamani hapo vielelezo vya
ushahidi wa kesi hiyo ikiwemo ripoti ya kitabibu iliyotolewa na mganga
aliyefanyia uchunguzi mwili wa marehemu mwangosi, kitabu cha kumbukumbu za kutoa
na kurudisha silaha kituoni, ripoti ya mtaalam wa milipuko, mahojiano ya ungamo
na onyo pamoja na gazeti la mwananchi la tarehe 3 septemba 2012 lenye picha ya
mtuhumiwa akiwa ameshikilia silaha aliyoitumia kumfyatulia marehemu
Hata hivyo mtuhumiwa licha ya kukiri kuwepo katika eneo la nyololo
wilayani mufindi siku hiyo ya tukio amekana shitaka hilo na kesi hiyo
imeahirishwa mpaka hapo itakapopangiwa siku ya kusikilizwa tena na mtuhumiwa
amerudishwa rumande
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mwandishi wa habari wa magazeti
ya Dairy News na Habari leo mkoani iringa Frank Leonard alikamatwa na polisi
kwa tuhuma za kupiga picha wakati mahakama ikiendelea ambapo alishikiliwa
kwamuda na baadae kufikishwa katika kituo cha polisi iringa kabla ya kuachiwa
bila kuandika maelezo.
mwisho
No comments:
Post a Comment