Wakiangali Mto Ruaha Mdogo
IRINGA.
SERIKALI imeagiza Baraza la Taifa la Mazingira NEMC kufanya
upya tathmini ya athali ya kimazingira katika eneo linalotarajiwa kujengwa
kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani katika manispaa ya Iringa huku pia
kiitaka Manispaa hiyo kusimamisha uendelezwaji wa eneo hilo kusubiri tathimini
hiyo.
Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira
Dokta Binilith Mahenge ametoa agizo hilo mjini Iringa mara baada ya kutembelea
na kukagua eneo hilo la Igumbilo lililotengwa na Manispaa ya Iringa kwa ajili
ya ujenzi wa kituo hicho cha mabasi na kuzusha mgogoro na wadau mbalimbali wa
mazingira.
Awali mkuu wa mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma , alimweleza Waziri
huyo kuwa kutokana na kukua kwa haraka na ongezeko la watu katika mkoa wa Iringa
manispaa inahitaji kuwa na kituo cha mabasi cha kisasa ili kutoa huduma
inayostahili kwa wasafiri .
Aidha aliongeza kuwa kutokana na uwepo wa chanzo cha maji katika
eneo hilo ni vema kufanya tathimini yakutosha ya athali za kimazingira ili
mradi huo usiathili mazingira na huduma nyingine.
kwa upande wake afisa wa maji bonde la rufiji Idris Msuya alisema
jiografia ya eneo hilo ni tata kutokana na sheria ya mazingira kutokuwa wazi
katika baadhi ya maeneo kwani eneo chepechepe katika eneo hilo la Igumbilo
limeendelea hadi nje ya mita zinazotajwa na sheria ya mazingira hivyo ni vema
kufanya tathimini inayotazama athali zote za kimazingira katika eneo hilo.
Ujenzi wa kituo hicho cha mabasi cha Igumbilo katika manispaa ya Iringa
umezua mgogoro baina ya mamlaka mbalimbali ikiwemo mamlaka ya maji na usafi wa
mazingira mjini Iringa IRUWASA, bonde la maji la Rufiji na wadau wa mazingira kwa
upande mmoja na manispaa ya Iringa iliyopitisha ujenzi wa kituo hicho zaidi ya
miaka sita iliyopita
MWISHO.
No comments:
Post a Comment