Saturday 22 February 2014

MWAKA WA KILIMO AFRICA UMEFANYIKA KANING'OMBE IRINGA.





VIONGOZI MBALIMBALI WAKIKAGUA MASHAMBA KATIKA KIJIJI CHA KANING'OMBE WILAYA YA IRINGA VIJJINI.


KANING’OMBE,
IRINGA
PAMOJA na uwepo wa ardhi ya kutosha na yenye rutuba kwa ajili ya kilimo nchi nyngi barani afrika zimeshindwa kufikia azimio la maputo la mwaka 2003 ambapo wakuu wa nchi za afrika walikubaliana kila nchi kutenga kiasi cha asilimia kumi ya bajeti ya kitaifa kwaajili ya maendeleo ya sekta ya kilimo

Hayo yalisemwa katika kongamano la kuzindua mwaka wa kilimo afrika lililofanyika katika kijiji cha Kaning’ombe mkoani Iringa ambapo mgeni rasimi makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Manzania Dokta Mohamed Gharib bilali aliwakishwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dokta Christine Ishengoma.
 Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la ANSAF Audax Rukonge walioandaa kongamano hilo alisema hadi sasa ni Nchi nane tu ndiyo zimeweza kufikia makubaliano hayo ya Maputo.
Rukonge alisema kuwa azimio hilo lilikubaliwa na viongozi hao na kuona
kuwa kinatosha kuchangia pato la pato la taifa na kuongeza uzalishaji
na kukuza sekta ya kilimo hapa nchini kwa asilimia sita ambapo
litawasaidia kuodokana na umasikini hapa nchini
.


Akizungumza kwa niaba ya makamu wa rais mkuu wa mkoa wa Iringa DK Christine Ishengoma alisema tatizo la pembejeo bado ni kubwa kwa wananchi wa kipato cha chini hasa maeneo ya vijijini hivyo ni vema serikali ikaangalia uwezekano wa kuagiza mitambo ya kilimo kama matrekta mapya na yaliyotumika ili kuwezesha wakulima kumudu kuyanunua.
kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Iringa bibi Wamoja Ayubu alisema kutokana na changamoto ya pembejeo za kilimo na mitaji mkoa wa Iringa wenye eneo la zaidi ya hekta 54 elfu zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji umeweza kutumia kiasi cha hekta 25 elfu sawa na asilimia 47 ya eneo lote.
Mmoja wa wakulima wa kijiji cha Kaning’ombe bwana Ausebio Mbangile akieleza athali za kukosekana kwa trekta la kulimia kijijini hapo alisema kuwa katika kilimo kimekuwa ni changamoto kubwa kutokana na
kukosekana kwa masoko, kukodisha matekta kwa bei kubwa, miundombinu pamoja na pembejeo kuwa bei kubwa na kushindwa kuzimudu.

Mbangile alisema kuwa pamoja na changamoto hiyo amekuwa akiuza gunia
lenye ujazo wa kilo 150  kwa shilingi 380,000 na kupata hasara kubwa
na hivyo kumrudisha nyuma kimaendeleo.


 MWISHO.



Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment