Tuesday 28 January 2014

Msaada kwa wahanga wa mvua na upepo mkali Izazi.




Iringa. zaidi ya kaya 23 ikiwemo shule ya msingi izazi zimeezuliwa na upepo kufuatia mvua iliyonyesha katika kijiji cha Izazi wilayani Iringa ikiambatana na upepo mkali na kusababisha wakazi hao kukosa mahari pa kuishi.
wamekabidhi msaada wa zaidi ya tani tano za chakula ikiwemo kilo mia tisa za maharage na lita sitini za mafuta ya kupikia kwa wahanga Benki ya NMB tawi la mkwawa mjini Iringa walisema kuwa wahanga hao walioezuliwa nyumba zao tarehe 12 mwezi huu kufuatia na mvua iliyonyesha pamoja na upepo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano meneja wa NMB tawi la Iringa Sumka Mbuba alisema msaada huo umetokana na benki hiyo kuguswa na kadhia waliyoipata wananchi wa kijiji cha Izazi hasa ikizingatiwa kuwa wakati huu ni wa kilimo ambapo wananchi hao wanatakiwa kuwa katika kazi za uzalishaji hivyo wameona haja ya kuwasaidia kuwapunguzia mzigo wa adha hiyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Iringa Steven Muhapa aliishukuru benki hiyo kwa kuitikia haraka ombi la halmashauri kuwaomba wadau mbalimbali kusaidia wananchi hao ili kuwafanya warudie katika hali yao ya awali .
Kwenyekiti wa kamati ya maafa Leonard Msigwa alisema kuwa hasara iliyotokana na maafa hayo ni zaidi ya shilingi milioni 30.
Mwananchi ilishuhudia baadhi ya wananchi wakiendelea na ukarabati wa kurudishia mapaa katika nyumba zao huku pia mafundi wakiwa kwenye harakati za kurudishia paa katika madarasa yaliyoezuliwa katika shule ya msingi izazi huku masomo yakiwa yanaendelea shuleni hapo ambapo walimu wamelazimika kutumia vivuli vya miti kama ofisi za muda baada ya ofisi yao kukumbwa  na dhahma hiyo
Mnyalu.

Moja ya nyumba ilio ezuliwa

Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment