MUFINDI KASKAZINI.
WANANCHI wa kijiji cha Ikweha wamewaomba baadhi ya viongozi
kutokuwa na mtazamo hasi kwa viongozi kwa kupandikiza chuki na kuwanyima fursa
vijana kutokana na ikitadi zao za kisiasa.
Hayo yalisemwa na Kabula Kidai wakati akisoma risala wakati wa fainali
za mashindano ya Mgimwa cup sambamba na
elimu ya stadi za maisha kwa Vijana vijijini chini ya ushirikiano wa Mufindi
youth and women for rulal development(MUYOWIRUDE ) na Mgimwa Foundation
yaliyofanyika katika kata ya Ikweha kijiji cha Ikweha wilayani Mufindi
kaskazini.
Kabula alibainisha kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakipandikiza
chuki kwa vijana na kuwanyima fursa zinazojitokeza pamoja na kuwapa elimu ya
ujasiliamali kwa manufaa yao binafsi.
Kwa upande wake mgeni rasimi mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarsta
Kalalu alisema kuwa elimu ya ujasiliamali itaepusha adha ya vijana wengi
kukimbilia mjini hivyo wajishughulishe na michezo na kuondokana na makundi
yasiyofaa na kukaa vijiweni.
“vijana wajiunge katika vikundi ili muweze kupata msaada wa kimaendeleo
kama mikopo,elimu ya ujasiliamali pamoja shughuli za kimaendeleo.
Sambamba na michezo wahudumu wa Afya ya msingi walitoa elimu ya
ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya ukimwi.
Jumla ya wananchi waliojitokeza kupima sabini na tano wanawake
arobaini na tano na wanaume
thelasini kati ya hao walio patikana na
maambukizi ni wanne mwanamke mmoja na
wanaume watatu.
Said Ng’amilo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment