Nahodha Willy Mkulu wa timu ya Ukeremi akipokea Zawadi ya ushindi wa pili kwa mashindano zenye thamani ya Tsh.350,000/=
Msanii wa muziki wa Bongo flevar akitumbuiza kwenye hafla ya kuwazadia washindi wa mashindano ya Mgimwa Cup
Mkuu wa wilaya Mufindi Bi Evarista kalalu akiongena wananchi wa kata ya Ikweha mufindi kaskazini
Nahodha wa timu ya Sinai akipokea zawadi ya mipira miwili kwa Mkuu wa wilaya Mufindi ikiwa ni zawadi ya Mshindi wa tatu katika yenye thamani ya Tshs 50000/=.
Picha zote na Mnyalu
MUFINDI.
WANANCHI wa kijiji cha Ikweha wamewaomba baadhi ya viongozi
kutokuwa na mtazamo hasi kwa viongozi kwa kupandikiza chuki na kuwanyima fursa
vijana kutokana na ikitadi zao za kisiasa.
Hayo yalisemwa na Kabula Kidai wakati akisoma risala wakati wa fainali
za mashindano ya Mgimwa cup sambamba na
elimu ya stadi za maisha kwa Vijana vijijini chini ya ushirikiano wa Mufindi
youth and women for rulal development(MUYOWIRUDE ) na Mgimwa Foundation
yaliyofanyika katika kata ya Ikweha kijiji cha Ikweha wilayani Mufindi
kaskazini.
Kabula alibainisha kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakipandikiza
chuki kwa vijana na kuwanyima fursa zinazojitokeza pamoja na kuwapa elimu ya
ujasiliamali kwa manufaa yao binafsi.
Kwa upande wake mgeni rasimi mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarsta
Kalalu alisema kuwa elimu ya ujasiliamali itaepusha adha ya vijana wengi
kukimbilia mjini hivyo wajishughulishe na michezo na kuondokana na makundi
yasiyofaa na kukaa vijiweni.
“vijana wajiunge katika vikundi ili muweze kupata msaada wa kimaendeleo
kama mikopo,elimu ya ujasiliamali pamoja shughuli za kimaendeleo.
Sambamba na michezo wahudumu wa Afya ya msingi walitoa elimu ya
ushauri nasaha na upimaji wa virusi vya ukimwi.
Jumla ya wananchi waliojitokeza kupima sabini na tano wanawake
arobaini na tano na wanaume
thelasini kati ya hao walio patikana na
maambukizi ni wanne mwanamke mmoja na
wanaume watatu.
Said Ng’amilo.
MWISHO.
MUFINDI.
TIMU ya mpira wa miguu ya Ugenza
imeibuka ushindi wa bao 2 kwa nunge dhidi ya timu ya Ukeremi katika fainali ya
kombe la Mgimwa cup lililomalizika jana katika kijiji cha Ikweha kata ya Ikweha
wilayani Mufindi.
Goli la kwanza lilifungwa
na mshambuliaji mahili kutoka timu hiyo Oscar mdema kunako dakika ya 35 katika
kipindi cha kwanza ambapo mshambuliaji huyo alipata pasi kutoka kwa kiungo
mwenye jezi 12 mgongoni Zamoyoni nyange na kupachika goli hilo.
Frenki kapende aliifungia
timu hiyo gori la pili kunako dakika ya 83 katika kipindi cha pili na
kusababisha mashabiki wa timu hiyo kuwanyenyua jukwaani na kushangilia ushindi kwa
furaha huku timu ya Ukeremi kunyong’onyea kwa kupachikwa mabao hayo.
Mpaka kufikia mwisho wa
mchezo timu ya Ugenza iliibuka ushindi na kujinyakulia zawadi ya seti ya jezi
za traki suti 16 na mipira miwili yenye thamani ya shilling laki tano,ikifatiwa
na timu ya Ukeremi ambapo ilipata full jezi na mpira mmoja zenye thamani ya
shilling laki tatu na elfu hamsini..
Mshindi wa tatu ambaye ni
timu ya Sinai ilipata mipira miwili yenye thamani ya shilling laki moja na elfu
hamsini,
Timu zilizoshiriki
mashindano hayo tangu mwanzo wa fainali hiyo zilikuwa sita ambazo ni Ugenza,Ukeremi,Uyela,Ikweha,Sinai,Ilangamoto
na hatimae kufika mwisho wa fainali zikiwa zimebaki timu nne ambapo timu ya
Ikweha na Ilangamoto kujitoa michezoni.
Michezo hiyo ambao ulizaminiwa
na Mgimwa Foundation chini ya ushirikiano wa Mufindi youth and women for
rulal development(MUYOWIRUDE) Kwa lengo la kuleta maendeleo vijijini kwa
vijana na kuwaepushia adha ya vijana wengi kukimbilia mjini ili hitimishwa .
MWISHO.
No comments:
Post a Comment