Saturday, 19 April 2014

MKUU WA MKOA IRINGA AHIMIZA WATOTO KUPEKWA CHANJO


Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii itaungana na nchi zingine katika kuadhimisha wiki ya chanjo Duniani kuanzia Tar 24-30/04/2014 kwampango huo Mkuu wa mkoa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto wate walio chini ya umri wa miaka miwili wakapate chanjo.

Nifursa pekee ilioje kupata chanjo mpya anyo husiana na kuzuia ugonjwa wa Nimonia na kuharisha kwa watoto hivyo nijuu yetu kuhamasisha jamii kufika katika vituo ili kupata maelezo zaidi
Pamoja na ujumbe :Jamii iliyokamilisha Chanjo ni Jamii yenye Afyanjema. 

Hapa Iringa wiki ya Chanjo itazinduliwa katika kijiji cha Ulata kata ya Wasa Tarafa ya Kiponzero katika halmashauri ya Wilaya Iringa vituo vitakuwa wazi kuanzia saa 2 as mpaka saa 11jioni
Nae mratibu wa huduma za chanjo mkoani Iringa Naftari Mwalongo alisema mwaka 2011 katika utoaji wa chanjo maalumu watoto 3962 walipewa chanjo katika mkoa wa Iringa.
Hivyo tunategemea mwakahuu kupata idadi kubwa zaidi
Chanjo ni jukumuletu sote ukizingatia magonjwa yanayo kingwa na chanjo hapanchini ni kwa sasa kifua kikuu,Donda koo,Kifaduro,Polio,Surua Pepopunda Homa ya Ini, Homa ya Uti wa Mgongo,Kichomi na Kuhara.
Mwisho nawatakia wananchiwote sikukuu njema ya Pasaka.
Mnyalu
Unknown Web Developer

No comments:

Post a Comment