1. WASIFU WA MAREHEMU
KUZALIWA
Marehemu
GERVAS
JOHN KALOLO alizaliwa tarehe 09.11.1964
katika Hospitali ya mkoa wa Iringa
2.
ELIMU
Marehemu
GERVAS
JOHN KALOLO alisoma shule ya
awali na msingi katika shule ya msingi CHEM
CHEM hapa iringa mjini na kuhitimu
mwaka 1980 na baadae aliendelea na masomo ya Sekondari katika shule ya Sekondari
HIGHLANDS na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1983.
3.
AJIRA
Mnamo
mwaka 1985 marehemu aliajiriwa katika kampuni ya IMAC ambako alifanya kazi kwa muda mfupi. Na baadae aliacha
kazi na kuamua kujishughulisha na
shughuli binafsi za Ujasiriamali na pia aliingia rasmi katika shughuli za
kisiasa.
4.
UONGOZI
KATIKA SIASA
Baada
ya kuingia katika siasa mnamo mwaka 2000 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa mtaa.Na ilipofika mwaka 2005 alichaguliwa
kuwa Mheshimiwa Diwani kupitia tiketi ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) mpaka mwaka 2010. Mwaka huo huo 2010 aliamua
kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mpaka umauti unamkuta alikuwa
mmoja wa viongozi wa CHADEMA hapa Iringa.
5.
UONGOZI
KATIKA KANISA
Marehemu
GERVAS KALOLO alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Miyomboni Parokia ya Consolata – Mshindo.
No comments:
Post a Comment