MBUNGE JIMBO LA KALENGA AANZA KUPAMBANA NA
CHANGAMOTO.
Mh Godfray Mgimwa mbunge wa Jimbo la Kalenga amefanya ziara ya kuwashukuru wananchi katika baadhi ya kata Jimboni humo pamoja na
kutoa vifaa vya ujenzi vilivyo ahidiwa na Mh marehemu Wiliam Mgimwa sambamba na yeye binafsi kutoa sehemu ya vifaa na kuahidi kuchangia
zaidi na kutatua changamoto Sawa na mahitaji sehemu husika.
Akiongea na wananchi wa kijiji cha Tanangozi ,Kiwere,
Itagutwa ,ibumila katenge na Mgama vilivyopo Wilaya ya Iringa Mh Godfray
Mgimwa alisema ameamua kufanya ziara mapema baada ya Kuchaguliwa
ilikutoa shukurani kwa wananchi waliomchagua katika uchaguzi uliofanyika 16/03/2014.
Mh Mgimwa alisema pamoja na kuwa zipo changamoto nyingi
katika maendeleo ataanza na baadhi sawa na umuhimuwake kwa nafasi yake yale
ambayo yanapaswa kufanywa na ngazi za juu atawasilisha kwa wahusika kama Raisi
na Mawaziri.
sambamba na hilo Mh Godfray Mgimwa ametoa ahadi ya bati
100 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Tanangozi ambayo wanakijiji wameanza
harakati za ujenzi Wakiwa wameisha andaa Tofari,Mawe na Mchanga ili kufanikisha
ujenzihuo juhudi zaidi zinahitajika toka kwa wana kijiji kwakuzingatia
kunampango wa kata ya Mseke kuwa kata mbili Mseke A na B.
Mh Mgimwa alisema amepokea kwa heshima kubwa kuchaguliwa
kwake pamoja na yote yaliojiri katika harakati za uchaguzi binafsi yeye atakuwa
pamoja na wananchi wa Kalenga kwahali na mali wakati wowote akiongea na
wananchi katika mkutano uliofanyika ndani ya Ofisi ya Kijiji cha Tanangozi.
Awali Mh Mgimwa amefanya kikao na Waheshimiwa Madiwani wa jimbo zima la Kalenga na kubadilishana nao
mawazo juu ya maendeleo ya Kalenga na Changamoto zilizopo katika kila kata
pamoja na kuangalia uwezekano wa kuondoa makundi ndani ya CCM Jimbo la Kalenga
ilikuwe na Mshikamano wa dhati kwamaendeleo ya Chama na Wananchi kwajumla.
Ziara yake hiyo
ilianzia katika Tarafa ya Kalenga kata ya Kiwere na kutoa Bati themanini zenye thamani ya
Tsh,1,400,000/= kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Kiwere na pia amekabidhi
bati Hamsini zenye thamani ya Tsh.875,000/= katika shule ya msingi Itagutwa.
Kwa upandewake Mgimwa
amekabidhi bati hamsini kwa ajili ya Ujenzi Shule ya Msingi Makota pamoja na kuahidi kuitembele Shule ya Msingi
Ugwachanya ambayo haina nyumba za waalimu na Madarasa yapo katika hali mbaya
ilikuona namna atakavyo shiriki .
SHULE ya Msingi Ibumila iliyopo katika kata ya Mgama
Tarafa ya Mlolo inakabiliwa na ukosefu
wa choo cha shule na kusababisha shule hiyo ufungwakwa
muda.
Akisoma taarifa ya kijiji mbele ya Mbunge wa jimbo la
kalenga Godfrey Mgimwa Diwani wa kata ya
Mgama Denisi Lupala alisema kuwa shule hiyo ilifungwa kwa muda kutokana na choo
hicho kutumbukia na kusababisha shule kukosa choo kabisa ingawa sasa wanafunzi
wanatumia choo cha muda wakati ujenzi unaendelea.
“licha ya shule ya msingi Ibumila kufungwa kutokana na
choo kutumbukia pia Kijiji hakijawahi kuwa na Zahanati vilevile kuna tatizo la Barabara inayo
unganisha kijiji hicho na kijiji cha Ilandutwa kuelekea Mufindi”alisema Lupala
Lupala aliongeza kuwa kijiji hicho kimekuwa katika
ujenzi wa nyumba ya mwalimu wa shule ya msingi Mgama kwa muda wa miaka saba sasa ikiwa na
ukosefu wa milango na madirisa hivyo wanaitaji msaada ili kufanikisha ujenzi
huo.
Kwa upandewake Mh Mgimwa alitoa simenti mifuko 30 yenye thamani ya Tsh435,000/=
kwa ajili ya ujenzi wa choo na zahanati huku akiahidi kuchangia kiasi cha
Tsh.milioni mbili kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.
pia alitoa Bati miamoja zenye thamani ya Tsh milioni moja laki saba na hamsini kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Waalimu Sekondari
ya Mgama
Mbunge a jimbo la Kalenga Mh Godfery Mgimwa ametoa bati
50 na mipira mitano yenye thamani ya shilingi million moja na laki moja katika isupilo kata ya Lumuli kwa ajili ya zahanati
ya kijiji hicho.
Awali akisoma taarifa ya kijiji hicho Edward Mbwilo mtendaji
wa kijiji cha Isupilo alisema kuwa kijiji hicho kinakabiliwa na ukosefu wa
zahanati ya kijiji ambapo ndio wapo katika harakati za ujenzi wa zahanati hiyo
pamoja na shule ya msingi..
Mbwilo alisema kuwa wanashukuru kwa msaada huo ambao
utawezesha kufanikisha zoezi la ujenzi huo pamoja na shule.
Kwa upande wake Mgimwa alisema kuwa kama mbunge
atafanya kazi kwa watu wote wa vyama vyote bila kubagua ili kupata maendeleo .
“mimi nachangia mabati 50 kwa ajili ya ujenzi wa
zahanati na mipira 5 kwa ajili ya vijana wa kijijini hapa ili kujishughulisha
na michzo hivyo basi naomba tufanye kazi kwa pamoja”alisema Mgimwa.
Aidha katka kijiji cha Muwimbi kilichopo kata ya Lumuli
tarafa ya kiponzelo Mgimwa alitoa mabati 80 yenye thamani ya shilingi mil 1 na
laki 4 kwa ajili ya ujenzi wa bweni katika shule ya sekondali ya Lumuli.
Diwani wa kata hiyo alisema kuwa wanakabiliwa na
ukosefu wa bati kwa ajili ya kuezeka bweli hilo ambalo tayari kijiji kimejenga
na kufikia hatua hiyo.
Aidha kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto ya
ukosefu wa umeme pamoja na daraja ambalo wanafunzi wanatakiwa kuvuka kwa kipindi cha mvua
wanafunzi wengi hushindwa kufika shule.
Mbunge huyo wa kalenga ameahidi kiasi cha shilingi million
1 kwa ajili ya vikundi sita vya vikoba vilivyopo kijijini hapo.
Katika kijiji cha Mibikimitali kata ya Ifunda alikabidhi
bati 50 kwa ajili ya ujenzi wanyumba ya mwalimu katika shule ya msingi mibiki
mitali kutokana ukosefu wa nyumba ya walimu katika kijiji hicho.
Aidha akisoma taarifa ya kijiji hicho Gervas Ndendya
kwa niaba ya afisa mtendaji alisema kuwa kijiji hicho kinakabiliwa na ukosefu
wa chumba cha kupumzikia wagonjwa katika zahanati ya kijiji hicho.
Ndendya alisema kuwa kijiji hicho pia kinakabiliwa na
ukosefu wa maji katika zahanati pamoja na matumizi kwa wanakijiji kwa sababu
kijiji hicho hakina kisima cha maji wala bomba.
Ukosefu wa umeme hivyo hulazimika kufanya kazi hasa usiku
kwa kutumia tochi hata katika huduma ya uzalishaji hivyo wanaomba kila nyumba
ifungiwe sola yake ili kurahisisha upatikanaji wa umeme katika zahanati.
Mnyalu.
No comments:
Post a Comment